Kwa mujibu wa taarifa ya waziri wa ulinzi nchini Liberia
Brownie
Samukai aliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, kwamba juhudi
za kimataifa za kupambana na ugonjwa huo hazina tija.
Shirika la afya duniani, limeonya kuwa maelefu ya visa vingine vya maambukizi huenda vikatokea nchini humo.
Nchi hiyo imeathirika zaidi kutokana na Ebola kuliko taifa lengine lolote kanda ya Afrika Magharibi.
Takriban watu 2,288 wamefariki kutokana na Ebola nchini Liberia, Guinea na Sierra Leone.
Shirika la afya duniani linasema kuwa nusu ya vifo vilivyotokana na Ebola vilitokea wiki tatu zilizopita.
Nchini Nigeria, watu wanane wamefariki kati ya 21 walioambukizwa ugonjwa huo.
Nako
nchini Senegal, mtu pekee ambaye alitambulika kuwa na ugonjwa huo
ametibiwa na kupona. Hii ni kwa mujibu wa maafisa wa afya nchini humo.
Mgonjwa huyo alikuwa mwanafunzi raia wa Guinea aliyepona kabisa ugonjwa huo baada ya kupokea matibabu.
Bwana Samukai alionya kuwa ugonjwa huo unasambaratisha kila sekta ya nchi hiyo
Mfumo duni wa afya nchini humo,tayari ulikuwa umezidiwa nguvu kuweza kukabiliana na janga la Ebola.
Bwana
Samukai aliambia baraza la usalama la Umoaja wa Mataifa kuwa Liberia
imekosa uwezo wa kimiundo mbinu na utaalamu pamoja na uwezo wa kifedha
kupambana na ugonjwa huo.
Ungana nasi FACEBOOK kujua mengi zaidi.
No comments:
Post a Comment