Monday, 8 September 2014

MAZIWA KUVIMBA NA KUUMA WAKATI WA UJAUZITO (Breast Tenderness &Pain)



Tatizo la kuvimba kwa maziwa na kuuma wakati wa ujauzito asa wa wiki 4 mpaka 6 linatokana na kuongezeka kwa hormone za progesterone na estrogen mwilini ambazo huongeza kasi ya mzunguko wa damu kwenye misuli lain ya maziwa.

MAMBO YA KUZINGATIA
Kitu cha kwanza kabisa ni kuzingatia kuvaa bra laini na inayokutosha. Mara nyingi wanawake wanaendelea kuvaa bra za zamani wakati maziwa yameongezeka. Hivyo wanakosa support ya kutosha. Uvaaji wa bra yenye support ya kutosha wakati wa mchana hata usiku utasaidia kupunguza maumivu na kukufanya uwe huru zaidi.  Pia usivae bra zenye chuma ndani(underwire, ukilala hakiksha unayapa support ya kutosha kwa kulala vizuri. 
Pia unaweza kuweka maji ya baridi, maji ya moto kiasi au weka barafu kwenye kitambaa halafu weka kwenye maziwa yaliyovimba ili kupunguza maumivu na uvimbe.

Usinywe kahawa au vinywaji vyenye cola vitazidisha uvimbe na kuuma. Jaribu kunywa chai maana majani mengi ya chai yana virutubisho vya potassium hii husaidia kupungza uvimbe na punguza chumvi kwenye vyakula. 
USIPITWE NA MENGI UNGANA NASI FACEBOOK KWA KULIKE UKURASA WETU HAPA 





 



 
 
 

No comments:

Post a Comment

.