Matatizo ya mirija ya uzazi kwa wanawake yapo wengi, mfano mirija
inaweza kuvimba na kupoteza uhalisia hivyo kushindwa kutungisha mimba.
Mirija inaweza kujaa usaha au maji. Tatizo hili ni kubwa lakini
ukifuatilia utakuta linaweza kuzuilika.
Kuziba kwa mirija ni athari za matatizo katika kizazi.
Jinsi tatizo linavyotokea
Matatizo katika mfumo wa uzazi huanzia aidha ukeni au ndani ya kizazi.
Maambukizi ya ukeni huweza kujipenyeza hadi ndani ya kizazi na
kushambulia tabaka la ndani ya kizazi na mirija.
Maambukizi
yanayoanzia ndani ya kizazi pia husambaa hadi ndani ya mirija. Mirija
hushambuliwa kwa ndani na nje ya kizazi. Ikishambuliwa kwa ndani
husababisha mirija kuziba na ikiwa nje ya mirija husababisha mirija
kujikunja.
Matatizo ya kuziba mirija hutokea pale mwanamke anapopata maambukizi
ya mara kwa mara ukeni yanayoambana na muwasho kutokwa na uchafu na
usaha ukeni, maumivu wakati wa tendo la ndoa na kutokwa na damu wakati
wa tendo la ndoa.
Maambukizi haya yasipotibiwa kikamilifu husambaa hadi katika mfuko wa
uzazi na kushambulia tabaka la ndani la kizazi na kusababisha tatizo
liitwalo ‘Endometriosis’ ambapo mwanamke hulalamika maumivu ya chini ya
tumbo au chini ya kitovu mara kwa mara, kutokwa na uchafu ukeni na
dalili nyingine tulizozielezea hapo awali.
Maambukzi toka ndani ya kizazi husambaa hadi katika mirija au chini
ya kitovu mara kwa mara, kutokwa na uchafu ukeni na dalili nyingine
tulizozielezea hapo chini.
Maambukizi toka ndani ya kizazi husambaa
hadi katika mirija ambapo hushambulia mrija mmoja au yote miwili, hapo
mgonjwa huendelea kulalamika maumivu chini ya tumbo au yanaweza kuwa
yamekwisha lakini maambukizi yaliyojipenyeza huweza kutafuna mirija na
kuziba au kusababisha usaha, maji na kuvimba.
Maambukizi yanaweza kutokea nje ya kizazi na mirija na kusababisha
mirija ijikunje na kuziba kabisa hali iitwayo ‘Adhesions’. Maambukizi
yanayoanzia ndani ya kizazi chanzo chake ni utoaji wa mimba au mimba
kuharibika.
Mirija inaweza kuziba ambapo itakatwa kwa lengo la kufunga uzazi,
inaweza kuziba kwa bahati mbaya wakati wa upasuaji wa kuondoa uvimbe
kwenye kizazi.
Upasuaji wa mirija kwa lengo la kuzibua pia inaweza
kuongeza tatizo kwani itatengeneza makovu ambapo mirija itaziba tena.
Maambukizi ya muda mrefu ukeni au katika mfumo wa uzazi huathiri mirija
ya uzazi.
Dalili za kuziba mirija
Mwanamke
anayedhaniwa mirija imeziba anakuwa na historia ya kutafuta ujauzito
kwa zaidi ya mwaka mmoja bila mafanikio.Historia hiyo inahusiana na kuwa
na historia ya kusumbuliwa na maumivu ya chini ya tumbo kwa muda mrefu
iwe yameshatibiwa au la.
Wengine wanakuwa na historia ya kuzaa angalau mtoto mmoja au zaidi
lakini anatafuta mwingine anashindwa kupata. Mwingine ana historia ya
kufanyiwa upasuaji wa tumbo.
Wengi wenye tatizo hili wana historia
ya kuharibikiwa na mimba au kutoa mimba hata moja tu inaweza kukuzibia
mirija yako ya uzazi. Endapo mrija mmoja utazibika kabisa basi unaweza
kuzaa hata watoto zaidi ya mmoja kwa kutumia mrija mmoja.
Nini cha kufanya?
Tatizo la kuziba kwa mirija linathibitishwa hospitali ambapo kipimo
kinachoitwa ‘HGS’ hufanyika ili kuthibitisha. Kipimo hiki ndicho
kinachoonyesha kwa usahihi jinsi mrija ulivyoziba, upo uzibaji ambao
mrija baadaye unaweza kurekebishwa na mwanamke akapata ujauzito. Picha
nzuri ndiyo itakayomuelekeza daktari jinsi ya kuurekebisha mrija.
Mrija ukiziba nusu yaani ukiachia nafasi kidogo kama hautarekebishwa
basi kuna hatari ya kupata mimba na ikabakia kukua kwenye mrija na
hatima yake ni mrija kupasuka na kuupoteza.
Muone daktari wa magonjwa ya kinamama na matatizo ya uzazi katika hospitali ya mkoa kwa uchunguzi na tiba utafanikiwa.
KUTOKA GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment