Tuesday 2 September 2014

KAMA UNASUMBULIWA NA MAUMIVU YA MGONGO

Maumivu chini ya mgongo hutokea sana kwa kila mtu na mara nyingi huwa ni chini ya mbavu za nyuma na juu ya miguu na huweza kusambaa mpaka kwenye kiuno na hips. Maumivu haya usikika na kuumiza pale unapoinua kitu, kusimama, kukaa kwenye kiti au kutembea na usababishwa na matumizi kupita kiasi ya misuli, kano, mishipa na neva za mgongoni au kwenye pingili za uti wa mgongo kutokana na kugandamizwa sana. Pia huweza kusababishwa na kuvunjika au maambukizi katika pingili za uti wa mgongo,  umri mkubwa, saratani ya mifupa,uzito kupita kiasi mawe katika figo, uvimbe na saratani ya kizazi .

TIBA YAKE
 Unaweza kujifanyia huduma ya kwanza mwenye kwa kutumia dawa za kupunguza maumivu, kuchua, kuweka barafu au joto kiasi, kufanya mazoezi mapesi na kukaa au kulala mtindo unaopunguza maumivu.
Punguza uzito, epuka kuanguka mara kwa mara  na usibebe mizigo mizito kupita kiasi au kaza sana tumbo unaponyanyua mizigo mizito
Usizunguke wakati au kuinamia mbele wakati umebeba vitu vizito
Usisimame kwa kubana miguu muda mrefu
Maumivu yakizidi fika hospitali ili kufanyiwa uchunguzi na vipimo vya X rays, CT scan na MRIs kwa ajili ya kugundua tatizo na kupata tiba zaidi.
USIKOSE KUTEMBELEA BLOG HII KILA SIKU KUJUA MENGI ZAIDI KUHUSU AFYA YAKO.


1 comment:

  1. Safi sana, zidi kutujuza na kutuelimisha kuhusu hili

    ReplyDelete

.