Sunday 7 September 2014

MATANGAZO YA TIBA ASILI YAPIGWA MARUFUKU

Baraza la Tiba za Asili na Tiba Mbadala Tanzania limesitisha vibali vya kurusha matangazo ya tiba za asili na mbadala kwenye vyombo vyote vya habari kwa kile kilichoelezwa kuwa yanapotosha jamii.

Taarifa iliyotolewa na kwa vyombo vya habari , imeeleza kuwa katika siku za karibuni kumekuwapo na matangazo mbalimbali ya tiba hizo ambayo baadhi yake hayaisaidii jamii.
Kutokana na taarifa hiyo ya baraza, vyombo vya habari havipaswi kupokea kibali chochote cha kutangaza matangazo ya tiba hizo hivi sasa, kwa kuwa ni batili.
Pia taarifa hiyo inaeleza kuwa, chombo chochote kitakachorusha tangazo au kipindi kitatozwa faini na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
naye mtaalam wa tiba asili, tabibu Rahabu Rubago ameiambia BBC kuwa hatua hiyo ya Baraza imetolewa bila wao kupatiwa taarifa hiyo mapema na kueleza kuwa watapata hasara kwa kuwa baadhi yao wametengeneza vipindi tayari kwa ajili ya kuvirusha kwenye vyombo vya habari.
IMETOKA BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment

.