Sunday 28 September 2014

MADHARA YA MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO(U.T.I) KWA MUDA MREFU.

Kuna madhara mengi yanayosababishwa na maambukizi katika njia ya mkojo au U.T.I kwa muda mrefu. Haya ni baadhi ya madhara hayo na unaweza kuyaepuka kwa kwenda hosipitali na kutibiwa au kubadili mfumo wa maisha.


Madhara ya kuugua U.T.I kwa muda mrefu na mara kwa mara ni pamoja na:-
Kushusha kinga ya mwili na kusababisha maambukizi ya zinaa, fangasi na magonjwa mengine.
Kuharibu kibofu na figo.
Kuna uwezekano wa mwanamke kujifungua mtoto mwenye uzito pungufu, njitiau mtoto mwenye maambukizi.
Kuharibu kizazi na kusababisha utasa.
Huweza kuingia kwenye mfumo wa damu(septicemia) na kusambaa mpaka kwenye ubongo na uti wa mgongo.
Kwa watu wzima huweza kusababisha makovu ya muda mrefu ambayo huziba mishipa ya damu na kusababisha presha au figo kutofanya kazi.
Ili kuepuka madhara haya unaweza kusoma hii  JINSI YA KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI HAYA

No comments:

Post a Comment

.