Ngiri au
Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za
tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini
kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha
viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.
Katika
mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni
maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia
ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji
(operesheni).
Tatizo
la ngiri huweza kumpata mtu yeyote. Miongoni mwa vitu vinavyoweza
kumsababisha mtu apate ugonjwa wa ngiri ni: Kuwa na uzito mkubwa wa
mwili au kuongezeka uzito kwa ghafla, kazi ya kubeba au kunyanyua vitu
vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu, ujauzito au
matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua pia kuharisha
au kuvimbiwa (Constipation). Vitu hivyo pamoja na mtu kuwa na misuli au
tishu zilizopoteza uimara au uwazi (opening or hole) humfanya mtu apate
ngiri (hernia).
Ngiri hutambuliwa kwa kutokea kitu kama
uvimbe au kujaa katika eneo husika (baadhi ya maeneo yametajwa hapo
juu) na pia kwa kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara na daktari
huwezesha kugundua tatizo hili.
Njia
inayoweza kutatua tatizo hili ni kwa mtu mwenye ngiri kufanyiwa upasuaji
ili kurekebisha misuli au tishu zilizolegea. Pia kutegemeana na
kihatarishi cha tatizo hili, mtu unaweza kuwa unafanya mazoezi ili
kupunguza uzito wako na kuweka utaratibu mzuri wa kula chakula
kinachojumuisha mboga mboga au matunda yenye nyuzi nyuzi (fibers), hii
itasaidia pia mmeng’enyo (digestion) wa chakula tumboni na kuepusha
kuvimbiwa. Matunda (Vitamin C) husaidia kuunganisha tishu zilizolegea na
pia husaidia kupona haraka kwa sehemu iliyofanyiwa upasuaji
(operesheni). Na kama tatizo lako ni la kukohoa kwa muda mrefu
kunakosababishwa na uvutaji wa sigara, ni vyema ukasitisha uvutaji ili
kupunguza madhara au makali ya ngiri lakini pia kusitisha sigara kwa
ajili ya usalama wa afya yako.
KUTOKA TANZLIFE COMPONY LIMITED
No comments:
Post a Comment