Thursday 4 September 2014

MAUMIVU YA TUMBO AMBAYO HUPASWI KUPUUZA

Kila mtu hupata maumivu ya tumbo kwa muda fulani ambayo huweza kusababishwa na tatizo dogo au kubwa kwenye mfumo wa chakula, uzazi au njia ya mkojo. Maumivu makali ya tumbo ambayo hayaishi kwa muda mrefu mara nyingi husababishwa na chakula kutomeng'enywa vizuri, kukosa choo kwa muda mrefu, saratani na maambukizi katika mfumo wa chakula uzazi au nyongo, hedhi kwa wanawake, tumbo kujaa gesi, aina fulani za vyakula, mawe katika figo, kidole tumbo na matatizo mengine mengi.
Watu wengi huchukua hatua ya kujitibu wenyewe ili kupunguza maumivu kwa kutumia dawa za kutuliza maumivu, barafu, maji ya moto na kukaa mtindo unaoondoa maumivu kwa muda mfupi. 
Yafuatayo ni maumivu ya tumbo usiyopaswa kupuuza na inakupasa kwenda hosipitali kwa uchunguzi na vipimo.
1. Maumivu ya tumbo yanayoambatana na kuharisha, kutapika na homa kali
2. Maumivu yanayoambatana na kutapika damu au kutoa haja kubwa yenye damu au ndogo yenye damu
3. Maumivu ya tumbo yanayoambatana na kukosa choo kwa muda mrefu
4. Maumivu ya tumbo yanayoambatana na kushindwa kupumua vizuri
5. Maumivu ya tumbo kutokana na kuumia au kupata ajali kabla
6. Maumivu yanayosababisha kiungulia cha muda mrefu kisichopona hata baada ya kutumia dawa.


No comments:

Post a Comment

.