Wednesday 24 September 2014

ONYO: MATUMIZI YA MIRUNGI NI HATARI KWA AFYA YAKO.

Vijana wengi wamejiingiza katika utumiaji wa madawa ya kulevya aina ya mirungi bila kujua madhara yake kiafya.Mirungi ni aina nyingine ya madawa ya kulevya. Mirungi huwa na majina mengine kama vile miraa, mbaga, mogoka, veve, gomba, kashamba. Ingawa imekuwa ni tamaduni kwa nchi za mashariki na saudia Mirungi  huathiri afya yako kwa kusababisha madhara yafuatayo:



  1. Magonjwa ya vidonda vya tumbo na mdomoni (peptic and oral ulcers);



  1. Ukosefu wa haja kubwa (constipation);



  1. Utumiaji wa muda mrefu husababisha kuharibu utendaji kazi wa ini, na pia kusababisha ubadilikaji rangi meno, kudhoofika, na fizi kuuma na harufu ya mdomo;



  1. Upungufu wa msukumo wa kufanya jimaa (sex drive). Na pia kuwahi kumaliza haraka na kutoweza kudumu kwenye tendo la ndoa kwa muda mrefu;



  1. Kupatwa na ugonjwa wa nyama au vidonda sehemu za haja  inayoota kwenye utupu wa nyuma;



  1. Upungufu wa usingizi;



  1. Humpelekea mlaji kutawaliwa nayo (Addiction);



  1. Walaji wengi huvuta na sigara, hata yule aliyekuwa havuti kabla ya kuanza kula Mirungi, hujikuta akizama kwenye uvutaji, na madhara huwa maradufu;



  1. Madhara ambayo bado kinamama walaji Mirungi hawajagundua ni kwamba mtoto anayezaliwa na mama mlaji Mirungi mara nyingi hukataa kunyonya titi la mama yake kwa sababu ladha ya maziwa inabadilika kwa ajili ya utumiaji wa madawa (pesticides) unaotumiwa na wakulima wa Mirungi kama inavyoeleza utafiti uliofanyika na Chuo Kikuu Cha Aden (Aden University). Utafiti huo unazidi kueleza ya kwamba aina ya madawa yanayotumiwa na wakulima ni zaidi ya 118 (na nyingi katika hizo ni katika zile zilizokatazwa kisheria [illegal pesticides]) na ambazo zinasababisha asilimia 70 ya ugonjwa wa saratani (cancer) huko Yemen.



  1.  Utafiti mwengine kule Ethiopia unatueleza ya kuwa mtoto wa mama mwenye kula Mirungi kwa wingi huwa hana uzito wa kawaida wakati wa kuzaliwa. 
  2. Ukosefu wa hamu ya kula chakula na mengi mengine.


LIKE PAGE NA WASILIANA NASI FACEBOOK KWA MSAADA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

.