Wednesday 24 September 2014

KAMA UNASUMBULIWA NA TATIZO LA KUKOSA HAMU YA KULA.

Kukosa hamu ya kula husababishwa na mambo mengi kiafya hasa uchovu uliokithiri, kushiba kupita kiasi, madawa ya kulevya, wasiwasi, hofu, mawazo, majonzi, ulevi, magonjwa na saratani.  Hali hii inaweza kusababisha kukonda na kupungua uzito pamoja na kushuka kwa kinga ya mwili hivyo kushambuliwa na maradhi.
Pamoja na kuwepo na tiba ambazo hutolewa hosipitali sambamba na mazoezi tatizo ili linaweza tibiwa kwa kutumia vyakula vifuatavyo:-


1. Epo, husaidia kuongeza njaa na hamu ya kula kwani huchochea tindikali katika tumbo ambazo hupeleka taarifa kwenye ubongo na kuisi njaa na hamu ya kula.
2. Limao na chungwa vina kiasi kikubwa cha lishe ya vitamini C ambayo huongeza hamu ya kula. Unaweza kula, kulamba au kutengeneza juisi yake kwa kuchanganya na asali.
3. Kitunguu swaumu, huamsha mfumo wa chakula kufanya kazi vizuri na kuongeza hamu ya kula. Unaweza kutafuna au kuunga kwenye chakula.
5. Zabibu, kula au kunywa juisi ya zabibu husafisha tumbo na kuongeza hamu ya kula.
6. Nyanya, unaweza kutengeneza kachumbari, au soup ya nyanya yenye mchanganyiko wa chumvi na pili pili huongeza hamu ya kula.
7. Mchanganyiko wa tangawizi, limao na chumvi kidogo katika tumbo ambalo halina chakula hasa wakati wa asubuhi uongeza hamu ya kula.
8. Supu ya mboga za majani pia huongeza njaa na hamu ya kula.
BOFYA HAPA KULIKE PAGE NA WASHIRIKISHE MARAFIKI

No comments:

Post a Comment

.