Wednesday, 24 September 2014

TATIZO LA KUTOKWA NA DAMU NYINGI AU HEDHI ISIYOFIKA KIKOMO.

Menorrhagia ni tatizo la hedhi isiyofikia kikomo zaidi ya siku 7 au kutokwa na damu nzito na iliyoganda kipindi cha hedhi. Hii husababishwa na mabadiliko yasiyo kawaida ya hormoni na matatizo mengine katika njia ya uzazi kama kuumia, maambukizi, saratani, kupungua au kuongezeka uzito kupita kiasi, mawazo na msongo wa mawazo au hasira kupita kiasi.

DALILI
Utaweza kujigundua kama una tatizo ili endapo:-
Unabadili pedi kila baada ya saa moja,
Unatokwa na damu nzito ambayo haizuiliki kwa pedi tu bali huitaji vifaa vingine au pedi nyingi.
Unatokwa na damu zaidi ya wiki moja na kuendelea.
Unatokwa na damu iliyoganda na nzito kupita kiasi.
Unatokwa na damu nyingi usiku kiasi cha kuchafua mashuka.
Una dalili za upungufu wa damu kama uchovu, kukosa nguvu na kushindwa kupumua vizuri.
NINI CHA KUFANYA.
Kula sana vyakula vyenye flavonoids na vitamini C kama machungwa, machenza, epo, pears, nanasi, zambarau n.k ambavyo hurekebisha mzunguko wa damu na matumizi ya madini ya chuma mwilini na kuzuia damu kutoka.
Kunywa chai yenye mchanganyiko wa asali na tangawizi hupunguza damu inayotiririka katika njia ya uzazi na kupunguza maumivu ya tumbo na nyonga kwa kuzuia hormoni ya prostagrandin ambayo husababisha maumivu.
Kula papayi kidogo inasaidia kulainisha kutanuka kwa mfuko wa uzazi na kupunguza damu.
Kula sana vyakula vyenye virutubisho vya magnesium na chuma kama tikiti maji, kakao, maboga, nyanya na juisi ya embe.
Nenda hosipitali kwa uchunguzi, vipimo na tiba iwapo:-
Tatizo ili linatokea kila mara unapoingia period
Tatizo ili halishi siku 7 baada ya kutumia tiba taja hapo juu.
Kama unatokwa na damu isiyokuwa ya kawaida au yenye harufu mbaya.
Kama unatokwa na damu inayoambatana na kuharisha, kichefuchefu na kutapika.
Una homa kali au dalili za upungufu wa damu.
BOFYA HAPA KULIKE PAGE YETU FACEBOOK NA WASILIANA NASI KWA MSAADA ZAIDI


 

No comments:

Post a Comment

.