Sunday, 7 September 2014

UNAWEZA KUEPUKA UZIWI UNAOSABABISHWA NA MATUMIZI YA EARPHONES/HEADPHONES

Tumezoea kuwaona watu wengi wakivaa wanaofanya kazi studio, viwandani, uwanja wa ndege na sehemu za ujenzi wakivaa headphones kwa ajili ya kulinda maskio yao. Matumizi ya muda mrefu ya earphones na headphones kwa ajili ya kusikiliza muziki na redio huwa na madhara makubwa na huweza kukusababishia ukiziwi wa moja kwa moja usipochukua hatua mapema.

HII IKOJE?

Sauti kubwa inayotoka kwenye earphones na kwa muda mrefu husababisha tetemeko kubwa katika ngoma ya sikio na mifupa laini ya sikio na kupeleka mawimbi makubwa ya sauti katika sikio la ndani na kuharibu moja kwa moja maji maji na vinyweleo ambavyo hupeleka taarifa kwenye ubongo na kusababisha kupoteza hali ya kusikia na uziwi wa moja kwa moja.
Njia sahihi ya kuepuka madhara haya ni kufungulia muziki wako kwa kiwango cha chini ambacho hakiwezi kuharibu masikio na kutumia aina za earphones au headphone ambazo zimetengenezwa kwa vichuja sauti ndani.
UNGANA NASI FACEBOOK

No comments:

Post a Comment

.