Saturday, 13 September 2014

FAHAMU KUHUSU DALILI, MADHARA NA TIBA YA KISONONO AU GONO



Kisonono ni ugonjwa wa zinaa unaoambukizwa, ugonjwa huu hutokana na wadudu aina ya Neisseria gonorrhoeae. Ugonjwa huu pia huambukizwa kwa tendo la ngono na hata kutoka kwa mama mjamzito anapojifungua huweza kumuambukiza pia mtoto endapo atakuwa alikuwa nao.


Ugonjwa wa kisonono kwa mara nyingi huwapata vijana na watu wazima. Waathirika wengi wa ugonjwa huu wa kisonono huambatana na magonjwa mengine ya zinaa, kwasababu kunabaadhi ya magonjwa mengine ya zinaa hujificha bila kuonyesha dalili, hivyo kukuta ukiugulia ndani kwa ndani.

Ugonjwa wa kisonono, unazuilika na kutibika pia, unaposikia dalili zozote za magonjwa ya zinaa, unashauriwa kumchukua mwenzi wakona kuwahi hospitali  kuchukua vipimo kwaajili ya matibabu.

DALILI ZA UGONJWA WA KISONONO.
Mara nyingi ugonjwa wa kisosnono huwa hauonyeshi dalili yoyote mwanzoni. Lakini ukionyesha dalili basi kwa mwanaume utasikia maumivu makali wakati wa kukojoa na kuambatana na usaha kutoka uumeni, kwa mwanamke pia dalili ni hizo hizo - maumivu wakati wa haja ndogo na kutoa usaha ukeni.

Usaha huo unaotoka uumeni au ukeni, huwa mzito na rangi ya kijani au njano, ambapo kwa mwanaume anaweza kuhisi maumivu katika korodani zake.
Kwa Wanawake maumivu yanaweza  kuwa chini ya tumbo, uchungu wakati wa ngono, na damu Isiyokuwa ya kawaida kutoka kwenye uke.
MADHARA YAKE
 Kama kisonono huenda kikakaa kwa muda mrefu mwilini  bila kutibiwa, inaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi ya afya na uzazi. Kwa wanaume, inaweza kusababisha makovu ndani ya njia ya mkojo, ambayo inaweza kusababisha maumivu wakati wa kukojoa. 

Kwa wanawake, kisonono kinaweza kusababisha zaidi kutoka eneo la uke na kusababisha papo hapo ugonjwa mwingine wa "pelvic inflammatory" (PID) - maambukizi katika maeneo mbali mbali ya uzazi, mimba kujishikiza nje ya kizazi na utasa.
 
Kwa wanaume na wanawake, kisonono  kisichotibika kwa muda muafaka, huenda huweza kuenea kupitia damu katika sehemu za mwili ambazo ni mbali na viungo vya uzazi, na kusababisha uvimbe katika viungo, ngozi, mifupa, tendons, moyo, au hata eneo karibu na ini.
MATIBABU YAKE
Tiba ya gono inahusisha na tiba ya ugonjwa wa Chlamydia kwani mara nyingi magonjwa haya huambatana kwa pamoja na hutegemea umri wa mgonjwa na kama mtu ni mjamzito au la. Tiba ya gono ambayo sio sugu iliyo kwenye shingo ya kizazi (cervix), urethra na puru,  hutumia mchanganyiko wa dawa jamii ya macrolides na penicillin wakati ile sugu hutumia sindano za powerself na mchanganyiko wa vidonge kwa maelezo ya daktari

JINSI YA KUJIKINGA
Tumia kondomu wakati wa kujamiana.
Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu.
Kuacha vitendo vya ngono kama matumizi ya vifaa vya ngono hasa kwa wanawake mfano vibrators nk.
Kwa wajawazito hakikisha unahudhuria kliniki mapema ili upate kuchunguzwa na kupatiwa tiba ili kuzuia mambukizi kwa motto ambayo huwa ni hatari sana.

No comments:

Post a Comment

.