Inatokea baadhi ya mikoa kuonekana kama ina idadi kubwa ya wagonjwa wa
akili kuliko mikoa mingine wapo wanaohusisha wagonjwa hao wa akili na
imani za kishirikina pengine bila kujua chanzo kinachopelekea maradhi
hayo kutokea.
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Magonjwa ya akili Dr.Frank Aloyce
Masao kutoka Muhimbili March 27 2014 alitoa taarifa na chanzo cha
magonjwa ya akili ambapo alianza kwa kusema>>’Kimsingi sababu
zinazosababisha magonjwa ya akili zimegawanywa katika makundi makuu 3′
‘Kuna kundi la kwanza ambalo ni kundi la kimwili sisi kitaalam
tunaita Biological reasons ambazo zinatokana na mtu mwenyewe kwa mfano
sehemu kubwa ya wagonjwa wa akili wana vina saba vinavyosababisha
maradhi ya akili, ugonjwa wa akili ni ugonjwa wa kurithi toka kwa mtu
mmoja kwenda kwa mwingine’
‘Ili ugonjwa wa akili uweze kutokea yapo mambo mengine
yanayosababisha ila kuna baadhi ya mambo tu yanaweza kuchangia mfano
akiugua ugonjwa kama Malaria, unakuta kimsingi mtu anakua mgonjwa hivyo
anapougua malaria au uti wa mgongo au maradhi mengine kama kifafa
yanaweza kusababisha ugonjwa wa akili’
‘Matumizi ya pombe ni miongoni mwa sababu zinazoweza kuchochea
ugonjwa wa akili ukaonekana kwa hivyo matumizi ya pombe,matumizi ya
bangi n.k. ni vizuri tukatambua matumizi ya vilevi hasa bangi sio sababu
hasa ya msingi ya kumfanya mtu akaugua ugonjwa wa akili’
‘Kimsingi mgonjwa wa akili anakua na vina saba vya ugonjwa wa akili
ila matumizi ya vilevi kama bangi na pombe vinaweza kuchangia kufanya
huo ugonjwa kuonekana, hii imekua ni sababu mojawapo inayochangia
unyanyapaa katika jamii’
‘Tathmini zetu zinaonyesha kati ya asilimia 3-5 ya wanaovuta bangi
wanaweza kupata maradhi ya akili wakati asilimia zilizobakia ambao
wanavuta bangi huwa hawapati maradhi ya akili, hii haimaanishi kwamba
naiambia jamii ivute bangi ila naiasa kujua si kila anayeugua ugonjwa wa
akili anatumia bangi’
‘Kundi la pili ni kundi la Saikolojia yapo matatizo mbalimbali ya
kisaikolojia yanayoweza kusababisha magonjwa ya akili kwa mfano mtu
aliyebakwa, mtu aliyefikwa na majanga, mtu aliyepata ajali siku za
nyuma, mikwaruzano katika ndoa, ugumu wa maisha na mahangaiko mbalimbali
yanaweza kuchangia mtu kupata maradhi ya akili’
‘Kundi la tatu ni la kijamii ambalo sababu za kijamii na za
kisaikolojia huwa zinaenda pamoja kwa maana zinahusiana zaidi na mambo
ya kimahusiano, kundi hili pia linaweza kusababisha mtu akapata maradhi
ya kiakili’.
LIKE PAGE NA WASILIANA NASI KWA MSAADA ZAIDI.
No comments:
Post a Comment