Tahadhari kwa wanaume wanaowatelekeza watoto wao nchini Kenya.Baadhi tayari wameanza kupata tumbo joto.
Kikundi cha wanaume
watatu nchini Kenya kimezindua ukurasa wa Facebook ambao lengo lake ni
kuwajibisha wanaume wasiotekeleza majukumu yao ya kuwalea watoto
wao.Mtandao huo unaitwa Deadbeat Kenya. Mtandao huo tayari umepata
mashabiki wengi sana huku baadhi ya wale walioaibishwa wekiwemo
wanasiasa, wanamuziki na watu mashuhuri. Kwa nini mwanamume mwenye
uwezo amtyelekeze mtoto wake? Baadhi ya wanaume wanalalamika kuwa
wanawake ni wajanja kwani wanashika mimba kwa njia za kijanja. Na
je Jackson Njeru mwanamume aliyeanzisha ukurasa huu wa Facebook hahofii
maisha yake? Hilo ni moja ya maswali aliyoulizwa na mwandishi wa BBC
Dayo Yusuf SOMA ZAIDI KUTOKA BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment