Friday, 12 September 2014

NJIA ZA KUPUNGUZA NA KUZUIA MAUMIVU YA KICHWA.

Maumivu ya kichwa hutokea sehemu yoyote ya kichwa na hutokana na itilafu katika misuli,mishipa ya damu na fahamu au viungo vyovyote vinavyozunguka ubongo. Mara nyingi maumivu haya huwa sio hatari sana japo humkosesha mtu raha. maumivu haya kuzuiwa na kupunguzwa kwa kufanya mambo yafuatayo kabla ya kwenda hospitali maumivu yanapozidi.


1. Tafuna pipi au peremende, husaidia kuongeza mzunguko wa damu kichwani na kwenye ubongo kwa kufungua mishipa ya damu na pua ili kupeleka oxygen ya kutosha kwenye ubongo.
2. Fanya masaji ya kichwa, kuanzia nyuma katikati mpaka mbele kwa kutumia mafuta laini usaidia kupumzisha kichwa na kulainisha mishipa ya damu na fahamu hivyo kupunguza maumivu ya kichwa.
3. Nusa maua yenye harufu laini na nzuri, na kuvuta hewa kwa kasi na kuibana kwa muda kidogo 4. inasaidia kupumzisha kichwa na kufanya moyo hupeleke damu ya kutosha kwenye ubongo na kupunguza maumivu.
5. Kula chakula, kunywa maji mengi na pumzika.
6. Fanya mazoezi laini na pumzika kupata hewa safi.
7. Kunywa juisi ya machungwa au mafuta ya samaki
8. Epuka vyakula na vinywaji vinavyoongeza maumivu na kula/kunywa vinavyopunguza maumivu 
LIKE PAGE NA WASILIANA NASI KWA MSAADA ZAIDI 

No comments:

Post a Comment

.