Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Moyo Marekani
(American Heart Association) unaonyesha kuwa mboga za majani na matunda
ni kinga sahihi ya kumwondoa binadamu kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa
kupooza.
Utafiti huo umekuja baada ya kubainika kuwa
ugonjwa wa kupooza umezidi kushika kasi hasa kwa mataifa ambayo yana
watu wenye vipato vikubwa.
Wataalamu walioshiriki katika utafiti huo
walieleza kuwa vitamin zilizopo kwenye matunda na mboga za majani zina
uwezo mkubwa wa kumwondoa mlaji kwenye hatari ya kupooza.
“Inaweza kuonekana ni kitu cha ajabu lakini ndiyo
ukweli ulaji wa matunda na mboga za majani ni kinga ya asili ambayo
inaweza kumwondoa binadamu katika hatari ya kupooza,” alisema Dk John
Baden.
Utafiti huo unaenda sanjari na ripoti ya Shirika
la Afya Duniani (WHO) ambayo inaeleza kuwa ulaji wa matunda na mboga za
majani unaweza kupunguza kasi ya ugonjwa huo kwa asilimia 19.
Nchini China ugonjwa wa kupooza unatajwa kusababisha vifo vya watu wengi kuliko magonjwa mengine.
No comments:
Post a Comment