Monday 15 September 2014

ZIJUE FAIDA KUMI ZA ASALI KIAFYA.


Kwa miaka mingi asali imekuwa ikitumika kiafya kwa ajili ya tiba asili ya magonjwa na matatizo mbali mbali kama maambukizi, kuungua, vidonda, makovu, uvimbe na maumivu. Zifuatazo ni faida kumi za asali kiafya:-

1. Asali ikichanganywa na maziwa usaidia kupunguza kiungulia.

2. Mchanganyiko wa asali na Limao kwenye chai husaidia kutibu kikohozi na maambukizi kwenye mfumo wa hewa.
3. Mchanganyiko wa asali na tangawizi huzuia kutapika kwa mgonjwa na mama mjamzito.
4. Asali ina kemikali za flavonoid na antioxidants zinazosaidia kuzuia magonjwa ya moyo na saratani.
5. Asali ina kemikali ya hydrogen peroxide ambayo husaidia kuua bakteria na fungasi mwilini.
6. Huwasaidia wanariadha kuongeza nguvu na kupata ahueni mapema kila baada ya kukimbia kwani ina kiasi kikubwa cha glycogen.
7. Asali huongeza kinga ya mwili kwa kuraisisha mfumo wa chakula na damu kufanya kazi vizuri.
8. Mchanganyiko wa asali na juice ya machungwa husaidia kuondoa hangover kwa mtu aliyekunywa pombe nyingi kwani ina sukari ya asili fructose ambayo husaidia ini kufanya kazi.
9. Huongeza uwezo wa akili kujifunza, kufikiria na kutunza kumbukumbu.
10. Mask ya asali usoni kwa muda wa masaa kadhaa husaidia kuondoa,  kuponya chunusi na kulainisha uso.
USIPITWE NA MENGI ZAIDI LIKE PAGE YETU FACEBOOK NA TUSHIRIKISHE FAIDA UNAYOIJUA WEWE.

 

No comments:

Post a Comment

.