Tuesday 16 September 2014

FAIDA AZIPATAZO MAMA ANAYEMNYONYESHA MTOTO


Miezi sita ya kwanza katika maisha ya mtoto mchanga chakula pekee ambacho wataalamu wa afya wanashauri apewe ni maziwa ya mama tu. Kunyonyesha ndio njia ya kwanza kabisa kumpa mtoto chakula. Unapoanza kumpa mtoto vitu vingine kama maziwa ya kopo wakati ana miezi michache utoaji wako wa maziwa unaathirika maana jinsi mtoto anavyonyonya ndivyo jinsi maziwa yanavyotengenezwa ndio maana watu wengi wanavyoanza kazi na kumuacha mtoto nyumbani maziwa yao yanaanza kupungua. Faida za kunyonyesha maziwa ya mama ni pamoja na:
SOMA NA HII TAHADHARI KWA WANAUME WANAOTELEKEZA WATOTO


  1. Maziwa ya mama yana virutubisho vingi vya asili ambavyo ni muhimu sana katika ukuaji na kinga kwa mtoto. Humlinda na magonjwa mengi ya utoto pamoja na ‘allergies’ mbalimbali.
  2. Hukuwezesha kuwa na ukaribu na mtoto wako.
  3. Hukupunguzia uwezekano wa kupata kansa ya matiti na kizazi.
  4. Ni bure na unaweza kumpatia maziwa wakati wowote bila usumbufu na ghalama.
  5. Maziwa ya mama ni raisi kupita kwenye mfumo wa chakula wa mtoto na umsaidia kuwa na akili nzuri
  6. Husaidia katika uzazi wa mpango   
  7. LIKE PAGE YETU FACEBOOK NA WASILIANA NASI KWA MSAADA ZAIDI 

No comments:

Post a Comment

.