Tume ya vyuo vikuu nchini Tanzania imesitisha udahili wa wanafunzi wapya
katika chuo kikuu cha IMTU kwa mwaka wa masomo 2014/15 na kukipa muda
wa miezi 3 chuo hiko kurekebisha kasoro zinazojitokeza mara kwa mara
ikiwemo kudahili wanafunzi wengi.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo Kaimu katibu
mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Prof. Magishi Mgasa amezitaja kasoro
nyingine zilizopelekea tume hiyo kukifungia udahili chuo hicho ni pamoja
na kuendesha program ya ngazi ya cheti bila ya ithbati ya TCU sambamba
na kukaidi agizo lilitolewa na Tume hiyo la kusitisha programu hiyo
Amesema katika kipindi cha miezi mitatu ambacho chuo hicho kitakuwa
kimesimamishwa kufanya shughuli za udahili TCU itakuwa ikikifuatilia kwa
karibu kuona iwapo chuo hicho kitatekeleza na kufuata taratibu
zinazotakiwa.
No comments:
Post a Comment