Monday, 22 September 2014

MAGONJWA KUMI HATARI USIYOPASWA KUPUUZA.

Mwili wa binadamu huwa na kinga kwa ajili ya kupambana na magonjwa mbalimbali, wakati mwingine kinga hizi hushindwa kufanya kazi kutokana na magonjwa ambayo ni hatari sana hivyo kuitaji tiba au msaada utakaokuwezesha kuishi na ugonjwa huo. Yafuatayo ni magonjwa kumi hatari usiyopaswa kupuuza katika maisha.


10. MALENGELENGE ni ugonjwa hatari sana ambao usababishwa na aina mbili za virusi(HSV-1 na HSV-2) na uambatana na dalili kama kutapika, homa kali, vipele au vidonda sehemu za siri na mdomoni. Ugonjwa huu usipotibiwa mapema husababisha virusi hawa kuharibu mishipa ya damu na kusabababisha kifo.
9.MAFUA MAKALI, Ugonjwa huu pia usabishwa na virusi vya mafua viitwavyo influenza A, B na C na usipotibiwa mapema huaribu mfumo wa upumuaji na kusababisha kifo.
8. EBOLA, ni ugonjwa hatari sana uliogundulika mwaka 1976 na usababisha vifo vingi kutokana na kuvuja damu ndani na nje ya mwili, kutapika na mfumo wa hewa kushindwa kufanya kazi.
7. KIPINDUPINDU, ni ugonjwa wa mlipuko ambao no hatari sana kwa kupoteza maisha ya watu wengi kutokana na upungufu wa maji mwili unaosababishwa na kuharisha, kutapika na kukaza kwa misuli.
6. MALARIA ugonjwa huu ni hatari sana kwani huathiri mzunguko wa damu, ini na mfumo wa fahamu kwa kasi zaidi kutokana na kuongezeka kwa vijidudu vya ugonjwa huu ambavyo husababishwa na mbu.
5. KUPOOZA, ugonjwa huu usababishwa na kupooza kwa mishipa ya fahamu katika ubongo na uti wa mgongo na kusababisha ulemavu wa viungo au vifo.
4. KISUKARI, tatizo kubwa la ugonjwa huu ni vigumu kuugundua mapema na hivyo uendelee kusababisha madhara mpaka pale unapogundulika huwa katika hatua mbaya inayosababisha magonjwa ya moyo, figo, upofu na hata kukatwa miguu.
3. PUMU ugonjwa huu ni hatari na humfanya mtu kuwa na aleji ya vitu vingi na uharibu mfumo wa upumuaji kutokana na kuvimba na kuziba kwa nja ya hewa, kukooa, maumivu makali ya kifua na kushindwa kupumua.
2. MAGONJWA YA MOYO, magonjwa ya moyo usababisha vifo vingi pale moyo na mishipa ya damu iaposhindwa kupeleka damu na hewa ya kutosha kwenye ubongo na sehemu mbalimbali za mwili
1. UKIMWI ugonjwa huu ni hatari sana kwani hauna tiba na usababishwa na virusi vya ukimwi kutokana na kushirikiana damu, vitu vyenye ncha kali, kufanya mapenzi bila kinga na mama kumwambukiza mtoto aliyeko tumboni na anayenyonya.
LIKE FACEBOOK PAGE NA WASILIANA NASI KWA MSAADA ZAIDI.

No comments:

Post a Comment

.