Wanasayansi wa chuo kikuu cha Oxford wameonyesha
ramani ya maeneo ambako wanyama huenda wana maambukizo ya virusi vya
ebola, ikiwa ni hatua ya kwanza kutabiri wapi ugonjwa huu utazuka hapo
baadaye.
Wasanyansi wanasema kuzuka kwa ebola huko Afrika Magharibi kulianza
wakati mtu mmoja alipokabiliana na mnyama aliyeambukizwa virusi hivyo.
Pengine mnyama huyo huenda akawa ni popo. Wanaweza kuwa na virusi hivyo
bila ya kuugua.
Dr. Nick Golding wa idara ya elimu ya wanyama katika chuo kikuu cha oxford anasema.
Dr. Golding anasema kuzuka kwa ebola kwa hakika kumewabainisha kwamba
unaweza kuwa nitishio la afya ya umma. Ebola ina hatua mbili.
Kimsingi, unaambukizwa kati ya wanyama huko msituni na unaweza
kuambukiza binadamu wanapokuwa na mawasiliano na wanyama hao. Maambukizo
ya aina hii ni kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu. Na halafu
kuna usambazaji wa pili, ambao unaonekana huko Ghana na maeneo mengine
ya afrika magharibi ambapo unaambukizwa kutoka kwa binadamu kwenda kwa
binadamu.
Anasema kusitisha mapema mlipuko wa ebola kwa binadamu ni muhimu
kufahamu maambukizo ya awali kutoka kwa wanyama. Ramani iliyotolewa
inaelezea takwimu ambako maambukizo ya binadamu na wanyama yametokea
tangu mara ya kwanza kuzuka kwa ugonjwa huo mwaka 1976.
Dr. Golding anasema kwahiyo ramani waliyoitengeneza inaonyesha
maeneo ambako wanadhani kuna hatari ya wanyama wenye maambukizo na hivyo
ni hatari kwa binadamu.
Ramani inaonyesha kwamba idadi ya wanyama walioambukizwa huenda
ikasambaa kote katika eneo kubwa la misitu huko Afrika ya Kati na
Magharibi.
Anasema bahati mbaya hakuna takwimu za kutosha, kuhusu mahali walipo
wanyama walioambukizwa au waliko binadamu ambao waliambukizwa siku za
nyuma. Kwahiyo anasema walichofanya ni kuangalia mwenendo wa mazingira
na kufananisha pale ambapo wamebaini kuwa mahusiano ya kimazingira –
kwahiyo kwenye misitu kwa kutumia picha za satalaiti na viwango vya hali
ya hewa na vigezo vingine. Anasema kimsingi wamefananisha sehemu
kulingana na mazingira sawa na maeneo yale ambako virusi vya ebola
vimegundulika kwa wanyama au binadamu wameambukizwa.
Mwasayansi wa Oxford anasema ramani hiyo inaonyesha maeneo makubwa
ambayo awali yalidhaniwa kuwa na wanyama waliombukizwa ebola.
Kwa mfano, katika ramani za awali haikufikiriwa kuwa eneo hilo
litakuwa afrika magharibi ambako mlipuko wa ebola umetokea hivi sasa.
Maeneo ambayo yalikuwa katika hatari kubwa ni afrika ya kati – ambako
ndiko mlipuko umetokea – huko jamhuri ya kidemokrasi ya congo.
Takriban watu milioni 22 wanaoishi katika nchi zilizoorodheshwa
katika ramani, golding anasisitiza kwamba licha ya mlipuko wa karibuni,
ebola bado ni maradhi yasiyo ya kawaida. Hata hivyo, baadhi ya maeneo
yako katika hatari kubwa zaidi kuliko mengine. Na golding anasema
kuelewa watu wapi wamekuwa na mawasiliano na wanyama wenye maambukizo ni
muhimu sana katika kuzuia kuzuka kwa ugonjwa huu hapo baadae.
Kwahiyo Dr. Golding anasema ramani kwa hakika inaonyesha pale ambapo
wanadhani huenda kuna wanyama walioambukizwa. Lakini hawana uhakika.
Kwahiyo jambo bora ambalo linaweza kufanya ni kuanza kuwachunguza baadhi
ya popo katika baadhi ya maeneo ambako ebola haijaripotiwa.
Anasema uchunguzi wa popo katika nchi ambako kesi za ebola hazijaripotiwa huenda ukaashiria hatari ya kuzuka kwa ugonjwa huo.
Katika maeneo hayo wanadhani kuna hatari, na katika nchi ambako
maambukizo kwa binadamu yameripotiwa, na kuongeza uwelevu ni jambo
muhimu sana katika mkakati wa kuzuia na kusitisha maambukizo ya mapema
hapo baadae.
Virusi vya ebola vimegundulika kwa popo wa aina tatu, lakini
wanasanysi hawajafuta uwezekano kuwa wanyama wengine huenda pia wakawa
wananvyo virusi hivyo.
CHANZO:VOA
No comments:
Post a Comment