Tuesday 2 September 2014

KAMA UNASUMBULIWA NA KIUNGULIA MARA KWA MARA


Kiungulia ni maumivu makali yanayochoma na kuuguza sehemu za koo au kifua. Maumivu haya huweza kusababishwa na matatizo kama vidonda vya tumbo, ujauzito, matatizo katika koromeo, aina fulani ya vyakula, sigara, pombe, uzito mkubwa na hernia ambayo husababisha tindikali inayosaidia mmeng'enyo wa chakula kutoka tumboni hadi kwenye koromeo na kusababisha maumivu haya.

MATIBABU YAKE
1. Epuka kuls chakula muda mfupi kabla ya kulala
2. Kula chakula kidogo na mara kwa mara wakati umekaa na sio kulala au kusimama.
3. Epuka unywaji wa pombe, uvutaji wa sigara, matumizi ya madawa ya kulevya na dawa zenye      asprini na kafeine
4. Tumia mito unapolala ili kuwezesha tindikali kubaki tumboni.
5. Kunywa maziwa kidogo au tafna bigiji, pipi au ndizi itasaidia kurudisha tindikali tumboni na    kuipunguza makali
 6. Punguza uzito na epuka nguo zinazobana sana tumboni.
7. Maumivu yakizidi tembelea hospitalikwa uchunguzi na tiba ambapo dawa za antacid, PPIs au nyinginezo huweza kutolewa na wataalamu wa afya kuondoa tatizo ili kutokana na nini kinachosababisha.
USIKOSE KUTEMBELEA BLOG HII KILA SIKU KUJUA MENGI KUHUSU AFYA YAKO.
 

No comments:

Post a Comment

.