Wednesday, 10 September 2014

HAYA NDO MADHARA YA KUPIGA X RAY MARA KWA MARA

Wengi wetu tumekuwa tukiandikiwa kipimo cha X ray kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa na matatizo mbalimbali na tumekuwa tukifanya mara kwa mara bila kujua madhara yake hivyo tunashauriwa kupiga picha hizi za x ray pale penye umuhimu tu na kwa maelekezo ya madaktari ili kuepuka madhara yatokanayo na teknologia hii ya mionzi mikali kama ifuatavyo:

1. Watoto wadogo wanapopigwa picha za X ray chini ya tumbo bila kuvaa nguo za kuwakinga na mionzi hii kuna uwezekano mkubwa wa kuharibu mfumo wao wa uzazi na hivyo kusababisha utasa maishani.
2. Mama mjamzito anapopigwa X ray tumboni kuna uwezekano wa kumuhathiri mtoto aliye tumboni asa kupata saratani ya damu, tezi, na magonjwa ya moyo na kisukari.
3. Kupiga X ray mara kwa mara uharibu na kusababisha kansa ya mifupa na ngozi
Kumbuka unapaswa kuongea na daktari wako mapema ili kuona kama kuna uwezekano wa kufanya vipimo vingine badala ya X ray au kuvaa vifaa vya kukukinga na mionzi kwa ajili ya kuepuka madhara haya.
UNGANA NASI FACEBOOK USIPITWE NA MENGI KUHUSU AFYA YAKO

No comments:

Post a Comment

.