Utendaji mzuri wa
ubongo unategemea uwiano katika kutuma ujumbe. Utumaji usio na udhibiti
hupelekea mlipuko wa umeme katika seli za ubongo ambapo huweza kupelekea
mtu kupata kifafa (seizure) hali ambayo huambatana na kupoteza
fahamu,kuzubaa,kukakamaamisuli, kuchanganyikiwa, kutokwa na haja ndogo au kuchezesha viungo
haswa mikono na miguu.
Sote tuko katika hatari ya kupata
kifafa.Kifafa chaweza tokea bila sababu dhahiri lakini watu waliowahi
kudhurika katika ubongo wako katika nafasi kubwa ya kupata kifafa. Kifafa
hurithiwi mara chache haswa kwa ndugu
ambao wana muathirika wa kifafa.
Nini cha kufanya iwapo mgonjwa wa kifafa amepatwa na kifafa
1. Ondosha vitu vyovyote vinavyoweza kumdhuru kama moto, mawe, visu n.k
2. Usimuhamishe kumpeleka mahala pengine
3. Mgeuze upande (kiubavu) ili kama kuna kimiminika chochote mdomoni kiweze kutoka ili kuepuka kuziba kwa njia ya hewa.
4. Toa nguo yoyote inayombana shingoni ili aweze kupumua vizuri
5. Kaa naye mpaka apate fahamu (yaweza kuchukua mpaka dakika kumi na tano)
6. Wasiliana na wataalamu wa afya au mpeleke hosipitali iwapo hajapata fahamu baada ya dakika 5 mpaka 10
7. Usimwekee kitu chochote mdomoni wa usijaribu kumzuia mgonjwa asirushe mikono au miguu
BOFYA HAPA KUUNGANA NASI FACEBOOK
No comments:
Post a Comment