Monday 15 September 2014

FAHAMU KUHUSU DALILI NA TIBA YA SARATANI YA DAMU(Leukemia)

Leukemia ni Saratani ya damu ambayo huanzia kwenye mafuta au urojo wa mifupa na kusababisha uzalishaji wa chembe hai za damu zisizo kawaida kwa wingi na kusababisha upungufu wa damu, kuvuja damu na mwili kushindwa kupigana na maambukizi mbali mbali. Saratani hii hauambukizwi bali hurithiwa kutokana na  mabadiliko katika DNA ambayo huathiriwa na mionzi mikali, maambukizi ya virusi, kemikali hatari na matumizi ya tumbaku na sigara kwa muda mrefu.
DALILI NA ISHARA 
Uvimbe shingoni, kwapani, sehemu ya kushoto ya tumbo na shemu za siri
Kutokwa na damu mara kwa mara puani, sehemu ya haja kubwa, na damu nyingi wakati wa hedhi
Homa za mara kwa mara na kutokwa jasho sana usiku
Maumivu ya mifupa
Kukosa hamu ya kula na kupungua sana uzito
Uchovu wa mara kwa mara
Michubuko na majeraha mengi kwenye mwili
TIBAYA UGONJWA HUU.
Matibabu ya saratani hii hutegemea aina ya saratani, kusambaa kwa saratani., umri na matibabu ya awali ambayo uhusisha dawa, mionzi, kuongezewa damu na kupandikiza. Tiba hizi huwa ni kwa ajili ya kupunguza dalili, kuua chembe hai zisizo kawaida na kuongeza kinga ya mwili.
 JINSI YA KUKABILIANA NA UGONJWA HUU.
Kula lishe yenye mboga za majani na matunda itasaidia kukinga mwili na magonjwa na kuongeza damu.
Tumia mafuta ya samaki yana omega-3 fatty acid ambayo huzuia uzalishaji  wa chembe za damu zisizo kawaida kwa wingi na kuruhusu zile za kawaida kwa ajili ya kulinda mwili.
Pata chanjo za mara kwa mara ili kuzuia maambukizi kwani saratani hii huvutia sana maambukizi kutokana na kushusha kinga ya mwili.
Fanya mazoezi mepesi mara kwa mara.
Pata msaada kutoka kwa wataalamu wa afya, ndugu jamaa na marafiki na usiwe mpweke muda mwingi.
Kunywa juisi glass moja kila asubuhi itasaidia kuimarisha mwili na kuongeza kinga.
Epuka matumizi ya pombe, sigara na tumbaku.
Kumbuka ugonjwa huu ni hatari hivyo jamii inabidi ichukue tahadhari kubwa, kwani inaelekea jamii haina kabisa uelewa wa ugonjwa huu na jinsi ya kukabiliana nao.
LIKE PAGE NA WASILIANA NASI FACEBOOK KWA MSAADA ZAIDI 



No comments:

Post a Comment

.