Friday, 26 September 2014

KAMA UNAOTA NDOTO MBAYA HIZI NDIZO SABABU NA TIBA.

Watu wengi husumbuliwa na tatizo la kuota ndoto mbaya usiku ambazo husababisha kujiskia vibaya, hasira na hofu iliyopitiliza. Tatizo ili sio la kuogopa ila huleta shida pale zinapomsababishia mtu kukosa usingizi, kushutuka usingizini usiku, kutokwa jasho na kuogopa kwenda kulala.

NINI USABABISHA?
Pamoja na kutokea mara nyingi kwa watoto tatizo ili pia husababishwa na kuchochewa na na mambo yafuatayo:-
Mawazo na hasira, juu ya kupoteza kazi, kuachwa, kufiwa, kufeli shule, kushuka kiuchumi n.k
Aina ya vyakula, kula sana na vyakula vyenye viungo na mafuta mengi kabla ya kulala huingilia utendaji wa kazi wa mwili na ubongo na kusababisha ndoto mbaya usiku.
Pombe na sigara, unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara kupita kiasi  kabla ya kulala usababisha kuota ndoto mbaya na kuamka katikati ya usingizi.
Kuumia, hii hutokea mara nyingi kwa watu waliopata ajali zinazohusisha viungo muhimu na ubongo.
Madawa, hasa matumizi ya dawa za presha, mawazo, kuacha kuvuta sigara, kifafa na ganzi kwa muda mrefu.
Magonjwa, kama homa kali, mafua makali, magonjwa sugu na magonjwa yote yanayoweza kuzuia usingizi na akili kufanya kazi vizuri.
TIBA YAKE.
Unaweza kujitibu mwenyewe kwa kuepuka mambo yanayosababisha hapo juu pamoja na kupunguza mawazo, hasira, hofu, kupata ushauri nasaa kwa wataalamu au kutibiwa magonjwa yanayoambatana na tatizo ili.
 Pumzisha mwili na akili kabla ya kula na unaweza kupumua kwa kina, kufanya masaji, kuoga maji ya uvuguvugu na kuongea au kulala na rafiki, mashuka au nguo unazopenda.
Waza juu ya mambo mazuri, sikiliza nyimbo ya taratibu, angalia muvi nzuri n ongea na rafiki yako kuhusu ndoto zako.
BOFYA HAPA NA LIKE PAGE KUJUA MENGI ZAIDI 




No comments:

Post a Comment

.