Monday, 1 September 2014

TATIZO LA KUTOKWA NA DAMU KWENYE FIZI

Mara nyingi kuvimba au kutokwa na damu kwenye fizi huweza kusababishwa na magonjwa mbalimbali ya kinywa na meno ambayo husababishwa na kutofanya vizuri usafi wa meno kwa usahihi  au maambukizi ya bakteria ambao usababisha utando mgumu kwenye meno. Utando huu hauwezi kutolewa kwa kupiga mswaki bali kwa kutumia vifaa maalumu na wataalamu wa meno. Pamoja na maambukizi au kutofanya usafi pia kutokwa na damu kwenye fizi usababishwa na magonjwa ya damu, kupiga mswaki kwa nguvu, ukosefu wa vitamini C na K.

FANYA YAFUATAYO KUJITIBU MWENYEWE
  • Tumia mswaki laini kusafisha meno kila siku na hakikisha unabadili mswaki kila baada ya miezi mitatu.
  • Usichokonoe meno mara kwa mara, ila tu baada ya kula ili kuondoa mabaki ya chakula. 
  • Matatizo ya hormoni asa kwa wajawazito.
  • Epuka uvutaji wa sigara na tumbaku ambao huchangia matatizo mengi ya kinywa na meno.
  • Epuka matumizi ya dawa za Aspirin ispokuwa kwa maelekezo maalumu na wataalamu wa afya
  • Kula mboga za majani, matunda na vyakula vyenye vitamini C na K kwa wingi
  • Tatizo likizidi onana na madaktari wa meno na kinywa  walau mara moja kwa miezi 6  kinywa kwa ushauri zaidi kuhusu dawa za kusukutua na kuua maambukizi, kuziba meno yaliyotoboka au kung'oa meno yaliyoharibika.

No comments:

Post a Comment

.