Samaki aina ya Goldfish,
anaendelea kupata nafuu baada ya
kufanyiwa upasuaji kutolewa
uvimbe kwenye ubongo wake.
Upasuaji huo umesemekana
kufanywa kwa uangalifu mkubwa
kutokana na hofu yatisho kwa
maisha ya Samaki huyo.
Samaki huyo kwa jina George,
ambaye mmiliki wake anaishi
Melbourne, alidunguwa sindano ya
kuondoa fahamu iliyogharimu dola
200.
Daktari Tristan Rich, aliyefanya
upasuaji huo, aliambia kituo cha
redio cha 3AW mjini Melbourne
kuwa Samaki huyo kwa sasa
amepata fahamu na tayari ameanza
kucheza na kuogelea majini.
Wataalamu wa matibabu ya
wanyama, wanasema kuwa Samaki
huyo mwenye umri wa miaka 10,
anatarajiwa kuiishi kwa miaka
mingine 20.
"George alikuwa na uvimbe mkubwa
sana kwenye ubongo wake na
alikuwa anakuwa polepole sana, na
hali hiyo ilikuwa inaanza kuathiri
maisha yake,'' alisema daktari Rich
kutoka hospitali ya matibabu kwa
wanyama ya Lort Smith.
Mmiliki wa George, alikuwa
ameambiwa achague kati ya Samaki
huyo kufanyiwa upasuaji au
adungwe sindano ya kulala.
Lakinin aliona bora kujaribu kuokoa
maisha ya Samakai wake na ndipo
akakubali Samaki huyo afanyiwe
upasuaji.
Aliongeza kuwa Samaki huyo alisalia
kuwa hai kutokana na madaktari
kuweka hewa ya Oxygen kwenye maji
wakati wa upasuaji.
Chanzo: BBC swahili
No comments:
Post a Comment