Wednesday 10 September 2014

UNAWEZA KUJIKINGA NA UGONJWA WA MAWE KATIKA FIGO (Kidney Stones)






Mawe ya kwenye figo siyo mawe halisi, bali huwa ni vitu vinavyojitengeneza kwenye figo taratibu na baada ya muda mrefu hugeuka umbo na kuwa mfano wa vijiwe vidogo na wakati mwingine huwa vikubwa mfano wa dole gumba. Hutokana na ulaji wa vyakula usio sahihi.
Tiba ya tatizo la mawe kwenye figo, mara nyingi huwa ni upasuaji wa kuvitoa na hugharimu fedha nyingi na pia husababisha maumivu wakati wa kufanya oparesheni hiyo. Lakini kwa kutumia tiba mbadala ya vyakula, unaweza kuondoa mawe hayo bila kufanya oparesheni.

 DALILI ZA KUWA NA MWAWE FIGONI
Dalili za awali za mtu mwenye mawe kwenye figo ni maumivu ya wastani au makali ya tumbo ya mara kwa mara. Pia mtu mwenye uwezekano wa kuwa na mawe kwenye figo huwa na tatizo la ukosefu wa choo kwa muda mrefu, tumbo kujaa gesi, kujisikia kushiba sana baada ya kula chakula  kidogo na kujisikia kichefuchefu mara kwa mara. Aidha, mtu mwenye tatizo la mawe kwenye figo, huwa hapatani na vyakula vyenye mafuta mengi, kwani anapokula hujisikia vibaya zaidi, husumbuliwa na kizunguzungu, Mkojo kutoka kwa kiwango kidogo au kutotoka, hupungukiwa damu mwilini na kuota chunusi usoni kwa wingi.

YANAYOWEZA KUSABABISHA MAWE KWENYE FIGO?
Kwa kiasi kikubwa, vijiwe husababishwa na kukosekana kwa usawa wa maji, madini na tindikali mwilini, ambayo kitaalamu huitwa electrolyte imbalance.
Kuna magonjwa kadhaa ambayo husababisha kwa kiasi kikubwa kutokea kwa hali hii kama ugonjwa wa utindikali kwenye mirija ya figo, matatizo kwenye tezi za shingo, kukojoa chumvi chumvi za oxalate kupita kiasi na hali ya nyama za figo kuwa tepetepe.
Kwa kawaida, kiwango cha sukari kinachotakiwa mwilini ni kile kisichozidi gramu 25 (sawa na kijiko kimoja kidogo cha chai) kwa siku, lakini kutokana na vyakula na vinywaji tunavyokunywa kwa siku, tunazidisha zaidi ya mara kumi ya kiwango cha kawaida. Ukiwa na staili ya maisha hayo, ujue uko hatarini kupatwa na tatizo kama hilo. Kwa akina mama, ulaji wa muda mrefu wa vidonge vya uzazi wa mpango, nao umetajwa kusababisha tatizo.
Kwa upande wa unga wa mahindi na ngano, tunapenda kutumia unga mweupe ambao umeshaondolewa viini lishe vyake vyote hivyo kukosa faida mwilini zaidi ya kufanya usagaji wa chakula tumboni kuwa mgumu na kusababisha ukosefu wa choo kwa muda mrefu.
Kitendo cha kukosa choo kwa muda mrefu wakati unakula na kunywa kila siku, ni dalili tosha kwamba vyakula unavyokula havina viini lishe na hivyo uko hatarini kupatwa na matatizo kwenye figo yako. Vile vile mtu kutokuwa na tabia ya kunywa maji mengi kila siku, huchangia ukosefu wa choo na matatizo kwenye figo.

TIBA MBADALA
Mtu unaweza kujikinga ili usipatwe na mataizo kwenye figo kwa kujiepusha na ulaji wa vyakula visivyokuwa na lishe.
 Weka tabia ya kula mboga za majani na matunda ya aina mbalimbali kila siku, pendelea kula ugali wa dona badala ya sembe nyeupe, epuka mazoea ya kuweka sukari nyingi kwenye chai au vinywaji vingine vinavyotumia sukari.
Epuka ulaji wa mkate mweupe na badala yake pendelea kula mkate mweusi au ‘brown bread’, epuka unywaji wa soda kila siku, kwani unapokunywa soda moja tu, unakuwa umezidisha sukari mwilini mara sita ya kiwango kinachotakiwa.

Kuwa na tabia ya kunywa maji mengi kila siku (angalau lita moja) hata kama husikii kiu, maji husaidia kusafisha figo pale unapoenda haja ndogo. Kwa ujumla, ukizingatia ulaji sahihi Mungu atakulinda na maradhi.
Kunywa mchanganyiko wa juisi za malimau na mzaituni kila siku kabla ya kulala na lala kwa kukunja miguu ili kurudisha mawe tumboni kwa ajili ya kutolewa kwa njia ya haja kubwa.
 

1 comment:

.