1. Chokolate, hurekebisha mzunguko wa damu na kuondoa mafuta
ambayo hayafai kwenye mishipa ya damu hivyo kukuepusha na shinikizo la damu. Ila
kula mara kwa mara itasababisha kuongezeka uzito.
2. Samaki kutoa baharini, asa wenye magamba ambao huwa na
virutubisho vya zinc vinavyosaidia kuimarisha misuli, moyo na utoaji wa mbegu
za kiume. Pia vyakula kama karanga, nyama ya ng’ombe na kukuk huwa na kiasi
kikubwa cha madini haya.
3. Parachichi, tunda ili huwa na mafuta mazuri ambayo husaidia
kuondoa mafuta yenye athari katika mishipa ya damu na hivyo kuzuia magonjwa ya
moyo.
4. Tangawizi, kutafuna tangawizi mara kwa mara hupunguza maumivu
ya misuli yanayotokana na kufanya kazi nzito au kuumia.
5. Maziwa, huwa na kiasi kikubwa cha protein na potassium ambayo
husaidia kujenga misuli imara. Pia ina bacteria
rafiki wanaosaidia kulinda mfumo wa chakula na kuzuia vidonda vya tumbo.
6. Ndizi mbivu, Ina virutubisho vya potassium ambavyo uimarisha
misuli, mifupa na kupunguza shinikizo la damu.
7. Nafaka, vyakula hivi huongeza nguvu na huwa na nyuzinyuzi
kusaidia kupata choo vizuri na kuimarisha mwili wako.
8. Tomato Souce ina virutubisho vya leukopene ambavyo ukulinda
dhidi ya saratani ya tezi ya kiume.
9. Mboga za majani na matunda, kama pilipili, machungwa, karoti, spinachi na maboga zina kemikali na
virutubisho vinavyosaidia kuongeza kinga ya mwili, kuzuia kuzeeka mapema na
kukukinga na saratani.
10. Mayai, yana virutubisho vya lutein, protini namadini ya
chuma yanyosaidia ukuaji wa chembe nyekundu za damu.
No comments:
Post a Comment