Sunday 14 September 2014

KUHUSU UGONJWA WA KASWENDE (Syphilis)

Ugonjwa huu nao husababishwa na bacteria Treponema Pallidum
Dalili zake hazionekani kwa urahisi. Huenda ukaanza kwa kijidonda au kipele kwenye uke au uume au sehemu ya kupitishia haja kubwa. Kidonda hiki kinapopona usidhani ndio mwisho wa maambukizo la! Viini hivyo vinaweza kubaki mwilini kimya kimya kwa miaka mingi!

Matibabu: Ni bora daktari kufanya uchunguzi wa damu kwani majimaji ya ukeni au uumeni huenda uchunguzi wake usionyeshe viini vya kaswende. Kaswende ni hatari, kama haitibiwi, inaweza kusababisha utasa au ugumba, na hata kuathiri moyo, mishipa ya damu, ngozi ya mwili, mifupa na hata ubongo na kurukwa na akili.
Hata hivyo matibabu yake ni rahisi – Zipo dawa aina (antibiotics) zinazoweza kutibu kaswende kabisa. Ili kuzuia kuenea kwa maradhi hayo ni vyema mpenzio nae pia atibiwe

USIPITWE NA MENGI BONYENZA HAPA KULIKE PAGE YETU FACEBOOK 

No comments:

Post a Comment

.