Friday 12 September 2014

MAMBO KUMI MUHIMU KATIKA KUDUMISHA MAHUSIANO.



Watu wengi wamekuwa katika hali ya kutafta na kujenga uhsiano wa muda mrefu lakini hushindwa kufanikiwa kutokana na kushindwa au kupuuza vitu vidogo mbele ya wapenzi wao na kushindwa kutambua kuwa mapenzi hayajengwi kwa kutumia nguvu na pesa bali kwa kufanya yafuatayo.


1. Mawasiliano ya mara kwa mara au kukaa pamoja kwa muda mrefu itawafanya kujenga na kupanga mipango ya baadae.
2. Ridhika, na kuwa na shukrani kwa kila kitu unachofanyiwa na mpenzi wako hata kiwe kidogo.
3. Angalia tabia yako na kuwa mwepesi wa kugundua kosa au kasoro na kujikosoa mwenyewe au kuomba msamaha.
4. Kuwa mbunifu na kumfanya mpenzi wako akuone mpya kila siku kwa kumfanyia mambo mapya.
5. Heshimu imani ya mwezio asa kuhusu dini na jifunze kujieleza mbele yake na kumsikiliza pia.
6. Epuka mabishano ya hasira yasiyo na msingi
7. Tambua kuwa mahusiano ya nje ya marafiki, majirani, mawifi, mashemeji na wakwe wana nafasi kubwa ya kujenga au kubomoa mapenzi yenu.
8. Jali usafi asa wa sehemu za siri na jifunze kuvaa nguo na vitu anavyopenda sana mwenzio.
9. Kumbuka kuwa zawadi ni muhimu sana katika mahusiano si lazima iwe ya ghalama bali kitu chochote kitakachomuonesha mwenzio kuwa unamjali.
10. Mwambie kiasi gani unampenda na mara kwa mara itasiadia kumuonesha kuwa unampenda na uanmjali.



No comments:

Post a Comment

.