Saturday, 27 September 2014

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO.

 SOMA NA VYAKULA VINAVYOFAA KWA MTU MWENYE VIDONDA VYA TUMBO.

Dalili za vidonda vya tumbo ni pamoja na maumivu makali au kiungulia maeneo ya chembe moyo (epigastic pains): Maumivu juu kidogo ya tumbo mara nyingi huendana na muda wa kula chakula. Mtu mwenye vidonda kwenye tumbo (gastric ulcers) hupata maumivu makali sana kipindi anapokula au mara tu baada ya kumaliza kula wakati aliye na vidonda kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (duodenal ulcers) hupata maumivu makali anapokuwa na njaa na hupata nafuu pindi anapokula. Dalili nyingine ni pamoja na:-


  • Kuvimbiwa au tumbo kujaa gesi. Hali hii pia yaweza kuendana na kubeua au kujamba mara kwa mara.
  • Kucheua na kuongezeka kwa mate yanayoshuka tumboni baada ya kucheua.
  • Kichefuchefu na kutapika
  • Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito
  • Kutapika damu
  • Kupata haja kubwa cha rangi nyeusi au kahawia chenye harufu mbaya sana. Hii humaanisha mgonjwa anapata haja kubwa au choo kilichochanganyika na damu kwa mbali
Uwepo wa dalili kama kiungulia cha muda mrefu, kucheua na kutapika baada ya kula na historia ya kutumia dawa za kupunguza maumivu (NSAIDs) kwa muda muda mrefu bila kufuata ushauri wa daktari ni ishara tosha ya kumfanya mgonjwa kumuona daktari kumpima na kumfanyia uchunguzi ili kujiridhisha kuwa hana tatizo la vidonda vya tumbo.
BOFYA HAPA KWA TIBA  

No comments:

Post a Comment

.