Sunday 28 September 2014

JITIBU UGONJWA WA MAWE KATIKA MFUKO WA NYONGO(Gallstones).

Ugonjwa huu unasabishwa na kuwepo au kutengenezwa kwa aina ya mawe katika kibofu au mfuko wa nyongo. Tatizo hilo linaonekana kuongezeka kwa kasi katika nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania, lakini linazisumbua zaidi nchi zilizoendela
Gallstones huwapata zaidi wanawake kuliko wanaume na zaidi walio na uzito mkubwa, wanene kupita kiasi wenye umri kati ya miaka 40 hadi 50 hivi.

DALILI
Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na maumivu ya mara kwa mara upande wa juu kulia katika tumbo. Maumivu haya huweza kuwa endelevu, huelekea pia upande wa kulia mgongoni au kwenye bega.
Kuhisi kichefuchefu mara kwa mara na kutapika, kushindwa kula chakula chenye mafuta, kupata homa, kubadilika na kuwa wa manjano. Ni muhimu mgonjwa anapopatwa na maumivu makali yasiyovumilika na homa, akimbizwa hospitali haraka iwezekanavyo na pale mgonjwa anapokuwa wa manjano pia ni muhimu akaenda hospitali mapema zaidi.
UCHUNGUZI
Vipimo vya mwanzo, ambavyo mgonjwa atahitajika kufanya ni kuangalia uwezo wa ini kufanya kazi kupitia kwenye damu, vipimo vingine ni ultrasound ya tumbo, Ct scan, MRCP-magnetic resonance cholangiopancreatography.
MADHARA YAKE
Matatizo makubwa yayoweza kuletwa na ugonjwa wa mawe katika kibofu cha nyongo na kuhatarisha maisha ya mgonjwa ni kama:
• Kupata homa kali na maumivu makali ya tumbo upande wa juu –acute cholecystitis, ambapo hupelekea mgonjwa kulazwa hospitali, kupangiwa upasuaji.
• Jiwe kutoka katika mfuko na kuingia katika mrija mkuu wa kusafirisha nyongo kwenda katika utumbo mwembamba na kuuziba mrija huo, hivyo mgonjwa kupata maumivu na kubadilika kuwa wa manjano (common bile duct calculi abstraction), upasuaji wa haraka huhitajika, au kutumia teknologia bila kupasua kwa kutumia kifaa maalumu kutoa jiwe hilo-ERCP hii niteknologia ya kisasa (hatuna huduma hii hapa nchini).
• Mfuko wa nyongo kutunga usaha (empyema/suppurative cholecystitis), au kutoboka, au kuoza na kuharibika kabisa( gangrenous gall balder), huhatarisha zaidi maisha ya mgonjwa.
• Jiwe kuteleza na kuziba mrija wa kongosho, hivyo kusababisha maumivu makali- acute caliculi pancreatitis.
• Mawe kusababisha kuwepo kwa saratani ya mfuko wa nyongo.
 MATIBABU
Katika kutibu ugonjwa huu, iwapo mawe mawe ni ya muda mrefu, mengi au kubwa, upasuaji wa kutoa mawe na mfuko wa nyongo huhitajika.
Upasuaji uhitajika pia pale mawe yanapoleta matatizo makubwa katika mwili (complications), mfano homa kali(acute cholecystitis, gall bladder empayema), upasuaji ndiyo njia bora ya kutibu ugonjwa wa mawe.
UNAWEZA KUJITIBU MWENYE NYUMBANI.
Kwa kutumia juisi ya Apple kila siku asubuhi ina tindikali aina ya malic inayosaidia kuyeyusha mawe haya kabla hayajawa sugu na kupunguza maumivu.
Kwa kutumia juisi ya mapea kila siku asubuhi pia usaidia kufunga mafuta yanayosababisha mawe haya na kuyatoa mwilini.
Kutumia juisi ya matango na  karoti husafisha mfuko wa nyongo na ini.
Kunywa maziwa kila siku huondoa sumu mwili na kudhoofisha mawe haya.
Pia unaweza kunywa maji lita 8 mpaka 10 kila siku, kubadili mfumo wa vyakula, kunywa juisi ya ndimu, na kula vyakula vyenye vitamin c kwa wingi.
LIKE PAGE NA UNGANA NASI FACEBOOK KWA MSAADA ZAIDI.

 
 

No comments:

Post a Comment

.