Thursday, 18 September 2014

CHANZO, KINGA NA TIBA YA HOMA YA MANJANO (Jaundice)

Homa ya manjano ni tatizo linaosababisha ngozi yako, midomo na sehemu nyeupe ya jicho kuwa ya njano kutokana na kuongezeka kwa rangi ya bilirubini katika damu inayotengenezwa kwenye ini baada ya kuvunjwa kwa seli nyekundu za damu. Hali hii inaweza kuambatana na kinyesi cheye rangi ya udongo mfinyanzi au kutoa mkojo mweusi, mwili kuwasha, kutapika kukosa hamu ya kula na uchovu. 

NINI USABABISHA
Tatizo ili sio ugonjwa bali ni ishara kuonyesha kuna kasoro inayo sababishwa na mojawapo kati ya yafuatayo:-
Ugonjwa sugu wa ini (Liver Cirrhosis)
Magonjwa ya damu na upungufu wa damu.
Homa ya ini
Kuziba kwa mirija ya nyongo
Kuwepo kwa mawe kwenye nyongo
Maambukizi na matumizi ya dawa za kutibu magonjwa mbalimbali kwa muda mrefu.
Kuvimba kwa ini kutokana na matumizi ya pombe na sigara kwa muda mrefu.
MATIBABU
Baada ya kufanyiwa uchunguzi na vipimo vya mkojo, ini, ultrasound, MRI tiba hufanyika kutokana na nini kinasababisha ambapo inaweza kuwa ni dawa, upasuaji au kuongezewa damu ili kuzuia tatizo la ini kushindwa kufanya kazi na kifo.
Tatizo ili pia linaweza kuzuiwa kwa kupata chanjo ya homa ya ini, kuepuka uvutaji wa sigara, pombe kupita kiasi na kupunguza uzito.
Kunywa juisi ya papai, nyanya au majani ya mpapai glasi moja kila siku asubuhi yana Lycopene ambayo huzuia kuharibika kwa ini.
Kausha na changanya majani ya matango kwenye chai mara 3 kwa siku au unaweza kula matango mara kwa mara.
Kunywa juisi ya majani ya kunde au mbaazi kila siku au unaweza kutafuna mbegu zake.
Pia juice ya miwa, limao na tangawizi ambazo zimetengenezwa nyumbani zitasaidia ini kufanya kazi vizuri
KWA TIBA NA USHAURI LIKE PAGE NA WASILIANA NASI FACEBOOK

 

No comments:

Post a Comment

.