Ngozi
yenye mafuta kwa kawaida huwa inang'ara, nene na yenye rangi
iliyotitia. Mara nyingi ngozi yenye mafuta mengi sana huwa na chunusi
nyingi na vipelepele na mara nyingine huwa na chunusi zenye vichwa
vyeusi. Katika aina hizi za ngozi mafuta hutokana na tezi za sebaceous
na kuzalisha mafuta zaidi ya kiwango kinachotakiwa. Mafuta hayo husambaa
katika ngozi na kuifanya iwe na mafuta mafuta.
Sababu zinazosababisha ngozi kuwa na mafuta:
• Kurithi.
• Lishe.
• Kiwango cha homoni mbalimbali mwilini.
• Ujauzito.
• Vidonge vya kuzuia mimba.
• Baadhi ya vipodozi .
• Hali ya unyevu (humidity) na hali ya hewa ya joto.
Namna ya kutunza ngozi zenye mafuta
Faida
kubwa ya kuwa na ngozi yenye mafuta ni kuwa haizeeki kwa haraka
ikilinganishwa na aina nyinginezo za ngozi. Miongoni mwa mambo
yanayosaidia ili kuitunza ngozi yenye mafuta na kuiepusha na chunusi na
hali isiyopendeza ni:-
1. Ngozi yenye mafuta inahitajia kusafishwa vyema kwa maji ya moto na sabuni ili kuzuia vinyweleo visizibwe na mafuta.
2.
Epusha vifaa vigumu visikwaruze uso wako na kupelekea ngozi kubanduka,
kwani suala hilo husababisha tezi za mafuta kufanya kazi zaidi ili
kujaza sehemu iliyopotea ya mafuta.
3. Epuka kutumia vipodozi ambavyo
huifanya ngozi yako ipotze maji au kukauka. Kwani husababisha sehemu ya
juu ya ngozi inyauke, na hivyo kusababisha mafuta kuziba vinyweleo na
kupelekea kutokea vichwa vyeusi.
4. Jitahidi kuitunza vyema ngozi
yako na kuisafisha vizuri. Jaribu kuosha uso mara mbili au tatu kwa
siku. Usioshe mara nyingi kwani kufanya hivyo huufanya uso kutoa mafuta
zaidi.
5. Chagua kile unachosafishia kwa makini, jiepushe kutumia
cream nzito nzito au vifaa vugumu wakati wa kuosha uso wako. Ni bora
utumie sabuni za kawaida zisizokuwa na madawa. Unaweza kutumia lotion ya
kuua bacteria au sabuni zisizo na dawa nyingi (lightly medicated), au
sabuni zenye madini mbalimbali. Ni bora usioshe au kutumia lotion au
michanganyiko yenye alkoholi.
6. Tumia maji ya moto au ya vuguvugu wakati unaosha uso wako.
7.
Wakati unapoosha uso wako, ukande kwa kutumia ncha za vidole, jiepushe
kupaka sabuni moja kwa moja usoni, inaweza kuganda na kuzuia vinyweleo
kuziba.
8. Kutumia mask za udongo (clay) na tope (mud) husaidia
katika ngozi za aina hii. Ni bora utumie mask mara moja au mbili kwa
wiki.
9. Jitahidi kutumia vipodozi vya uso ambavyo vimetengenezwa kwa ajili ya ngozi yenye mafuta.
No comments:
Post a Comment