Wednesday 25 June 2014

Ugonjwa hatari wa moyo(Acute coronary syndrome)




Ugonjwa hatari wa moyo (ACS) ni seti ya ishara na dalili zinazohusiana na kupungua kwa damu inayoingia kwenye misuli ya moyo na kusababisha anjaina na shambulio la moyo (heart attack)
Baadhi ya dalili za ugonjwa kali wa moyo ni pamoja na anjaina isiyo thabiti na aina mbili ya uinifarakti wa misuli ya moyo ambapo misuli ya moyo huaribika. Aina hizi hupewa majina yake kulingana na matokeo ya mchoro uchunguzimeme wa moyo (ECG / EKG) kama infarkteni ya misuli ya moyo pasipo mwinuko wa miokadia infakti ST(NSTEMI) na infarkteni ya misuli ya moyo iliyo na mwinuko wa sehemu ya ST(STEMI).  Kunaweza kuwa na baadhi ya tofauti kuhusu aina za MI ambazo zaweza kuunganishwa na ugonjwa kali wa moyo.

TATIZO LA VIDONDA MDOMONI



Vidonda mdomoni  husababisha sana maumivu makali  pamoja na kumfanya mtu asiweze kuongea vizuri na watu.Vidonda hivi  husababishwa na kutafuta kwa muda mrefu hasa bigijii au kitu chochote,  uvutaji wa sigara,maambukizi ya virusi, bakteria na fungasi sambamba na ukosefu wa madini   na virutubisho vya folic, zinc, vitamin c,vitamin B12, na madini ya chuma.

Monday 23 June 2014

UMUHIMU WA MBOGA ZA MAJANI KATIKA KUPAMBANA NA MAGOMJWA!


Mboga za majani zina virutubisho na madini mbalimbali ambayo ni muhimu katika kujenga mwili na kuulinda dhidi ya magonjwa sugu kama saratani na magonjwa ya moyo. Mwongozo wa lishe bora unaelekeza zaidi utumiaji wa mboga za majani na matunda kama kabichi, mchicha, spinachi, ndizi  majani ya maboga, karoti na mboga nyingine za majani zenye virutubisho kama vitamini A, C, D, K, madini ya chuma. folate na niasini ambayo hulinda mwili dhidi ya saratani, magonjwa ya moyo na kiharusi.

Two Genes Abnormalities That Cause Squamous Cell Lung Cancer Discovered

For patients with squamous cell lung cancer, the 5-year survival rate stands at only 15%. Because the disease is poorly understood, finding ways to treat the condition has proved problematic. But now, researchers from the Huntsman Cancer Institute at the University of Utah have discovered two gene abnormalities that contribute to the development of the cancer - a discovery they hope will pave the way for new treatment strategies.

Monday 16 June 2014

TAHADHARI KWA WATUMIAJI WA NYAMA YA KUKU

Wachinjaji wa kuku na watumiaji wa nyama ya kuku mnatahadharishwa kuwa makini mnapoosha nyama ya kuku kwani kuna uwezekano wa kuambukizwa ugonjwa wa tumbo maarufu kama food poisoning ambao husababiswa na bakteria aina ya Campylobacter jejuni. Ugonjwa huu husababishwa na bakteria hawa wanaopatikana kwenye nyama mbichi ya kuku na dalili zake ni pamoja na maumivu makali ya tumbo, kuharisha,kutapika, homa kali na kujiskia vibaya baada ya kutumia nyama ya kuosha au kutumia nyama ya kuku isiyo iva vizuri.
SOMA ZAIDI:http://www.bbc.com/news/health-27832220



KWA MSAADA ZAIDI BONYEZA HAPA AU ACHA COMMENT YAKO CHINI

ZINGATIA YAFUATAYO KAMA UNASUMBULIWA NA UGONJWA WA SHINIKIZO LA DAMU (HIGH BLOOD PRESSURE)

Shinikizo la damu ni ugonjwa ambao huweza kuleta madhara makubwa kwa afya ya binadamu endapo hutochukua tadhari juu ya kuishi, kuzuia na kuponya ugonjwa huu. Madhara haya nepuka madi pamoja na mishipa ya damu kuwa migumu kupitisha damu, mapigo ya moyo kubadilila, figo kushindwa kufanya kazi na hatimaye kifo. Ili kuepuka madhara haya mgonjwa wa presha anatakiwa kufanya yafuatayo ili kulinda afya yake.
Punguza kiasi cha chumvi au usitumie chumvi kabisa, hii itakusaidia kupunguza shinikizo la damu la juu na hatimaye kurudi katika hali yake ya kawaida.
Jitahidi kupunguza uzito, unaweza kutambua uzito wako wa kawaida na usio kawaida kwa kushirikiana na daktari wako, kufanya mazoezi na kula mlo kamili.
Fanya mazoezi mara kwa mara, hii inahusisha mazoezi rahisi na  yenye mpangilio kama ulivyoshauriwa na daktari walau mara 5 kwa wiki. Unaweza kujiunga na vikundi mbali mbali vya mazoezi au kutembea dakika 30 kila siku.
Punguza au epuka matumizi ya pombe na kahawa,  hii itakusaidia kudhibiti ongezeko la presha kwani husababisha kuongezeka kwa shinikizo la damu.
Kula chakula bora kwa afya bora, hapa kula zaidi vyakula vitokanavyo na matunda, mboga za majani nafaka, nyuzi nyuzi pamoja na maji kiasi, punguza vyakula vyenye mafuta.
Punguza au epuka uvutaji wa sigara na tumbaku, hii itakusaaidia kupunguza shinikizo la damu pamoja na matatizo mengine ya kiafya kama saratani n.k
Jitahidi kupima presha yako mara kwa mara, lengo ni kugundua mabadiliko na maendeleo kama inapanda au kushuka. unaweza kutembelea hospitali au vituo vidogo vya afya au kuwa na mtu maalumu kwa ajili ya kuepuka madhara makubwa yanayosababishwa na shinikizo la damu na hakikisha iko chini ya 140/90 mm Hg
Tumia dawa za kupunguza na kushusha presha, kila siku kama ulivyoelezwa na daktari na kama una wasi wasi kuhusu dawa zako ongea na daktari mapema kwa maelezo zaidi.


KWA MSAADA ZAIDI BONYEZA HAPA AU ACHA COMMENT YAKO CHINI
 
















Tuesday 10 June 2014

MATUMIZI YA SIMU YANAVYOWEZA KUSABABISHA UTASA

Utafiti unaonyesha kuwa wanaume wengi wako katika hatari kubwa ya kukosa kizazi kutokana na matumizi mabovu ya simu za mkononi. Hii huwaathiri sana wanaume wanaobeba simu kwenye mifuko ya nguo za ndani au kuziacha kwenye mifuko ya suruali zinazobana kwa muda mrefu.

UMUHIMU WA NYANYA KATIKA KUZUIA MAGONJWA YA MOYO

Pamoja na nyanya kuwa kiungo muhimu sana katika mbonga na vyakula mbalimbali pia zina uwezo wa kuzuia magonjwa ya moyo, mshutuko na kiharusi.

UTAFITI: WATOTO WENYE WAZAZI 3 KUZALIWA KARIBUNI

Wanasayansi nchini Uingereza wanasema kuwa inawezekana kwa wao kuwazalisha watoto kutoka kwa wazazi watatu katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
Wanasayansi hao wanasema kuwa wanasubiri mabadiliko katika sheria na badiliko katika mtazamo ya watu kabla hawajapandikiza manii kwa mayai kutoka kwa wanawake wawili .

MAZOEZI YA VIUNGO HUWEZA KUPONYA SARATANI YA MATITI

Watafiti wa Marekani, katika ripoti waliyochapisha katika jarida linaloandika mambo ya saratani, wanasema kuwa inajulikana wazi kwamba kufanya mazoezi ya aina moja au nyingine kunasaidia lakini imegunduliwa kuwa wanawake hawapendi kufanya mambo yanayowachosha.

.