Monday, 23 June 2014

UMUHIMU WA MBOGA ZA MAJANI KATIKA KUPAMBANA NA MAGOMJWA!


Mboga za majani zina virutubisho na madini mbalimbali ambayo ni muhimu katika kujenga mwili na kuulinda dhidi ya magonjwa sugu kama saratani na magonjwa ya moyo. Mwongozo wa lishe bora unaelekeza zaidi utumiaji wa mboga za majani na matunda kama kabichi, mchicha, spinachi, ndizi  majani ya maboga, karoti na mboga nyingine za majani zenye virutubisho kama vitamini A, C, D, K, madini ya chuma. folate na niasini ambayo hulinda mwili dhidi ya saratani, magonjwa ya moyo na kiharusi.

Pia watu wenye magonjwa sugu hunufaika na ulaji wa mboga za majani na matunda kwa kuongeza virutubisho, madini na nyuzinyuzi ambavyo hurekebisha mfumo wa chakula, damu na kupunguza uwezekano wa kushambuliwa na magonjwa ya moyo na upungufu wa damu.
Mboga za majani pia zina madini ya potasiumu ambayo hurekebisha mzunguko wa damu katika mishipa na moyo na kuzuia ugonjwa wa presha ya kupanda.

Virutubisho katika mboga za majani pia huongeza na kukuza kinga ya mwili ili kuzuia na kuondoa maambukizi hatari katika mwili sambamba na ukuaji mzuri wa ngozi kutokana na kuwepo kwa antiokdanti, fati asidi na vitaminis ambazo huzuia mawazo, magonjwa ya moyo, ngozi na mifupa.
Kwa mama mjamzito mboga za majani husaidia kudumisha afya ya mifupa na kuzuia kasoro za uzazi kwa mtoto aliyeko tumboni.

  Kumbuka unaweza usifurahi mboga za majani kama unavyofurahia matunda lakini bado ni muhimu sana katiaka kulinda mwili wako kama yalivyo matunda.


KWA MSAADA ZAIDI BONYEZA HAPA AU ACHA COMMENT YAKO CHINI

No comments:

Post a Comment

.