Monday, 16 June 2014

ZINGATIA YAFUATAYO KAMA UNASUMBULIWA NA UGONJWA WA SHINIKIZO LA DAMU (HIGH BLOOD PRESSURE)

Shinikizo la damu ni ugonjwa ambao huweza kuleta madhara makubwa kwa afya ya binadamu endapo hutochukua tadhari juu ya kuishi, kuzuia na kuponya ugonjwa huu. Madhara haya nepuka madi pamoja na mishipa ya damu kuwa migumu kupitisha damu, mapigo ya moyo kubadilila, figo kushindwa kufanya kazi na hatimaye kifo. Ili kuepuka madhara haya mgonjwa wa presha anatakiwa kufanya yafuatayo ili kulinda afya yake.
Punguza kiasi cha chumvi au usitumie chumvi kabisa, hii itakusaidia kupunguza shinikizo la damu la juu na hatimaye kurudi katika hali yake ya kawaida.
Jitahidi kupunguza uzito, unaweza kutambua uzito wako wa kawaida na usio kawaida kwa kushirikiana na daktari wako, kufanya mazoezi na kula mlo kamili.
Fanya mazoezi mara kwa mara, hii inahusisha mazoezi rahisi na  yenye mpangilio kama ulivyoshauriwa na daktari walau mara 5 kwa wiki. Unaweza kujiunga na vikundi mbali mbali vya mazoezi au kutembea dakika 30 kila siku.
Punguza au epuka matumizi ya pombe na kahawa,  hii itakusaidia kudhibiti ongezeko la presha kwani husababisha kuongezeka kwa shinikizo la damu.
Kula chakula bora kwa afya bora, hapa kula zaidi vyakula vitokanavyo na matunda, mboga za majani nafaka, nyuzi nyuzi pamoja na maji kiasi, punguza vyakula vyenye mafuta.
Punguza au epuka uvutaji wa sigara na tumbaku, hii itakusaaidia kupunguza shinikizo la damu pamoja na matatizo mengine ya kiafya kama saratani n.k
Jitahidi kupima presha yako mara kwa mara, lengo ni kugundua mabadiliko na maendeleo kama inapanda au kushuka. unaweza kutembelea hospitali au vituo vidogo vya afya au kuwa na mtu maalumu kwa ajili ya kuepuka madhara makubwa yanayosababishwa na shinikizo la damu na hakikisha iko chini ya 140/90 mm Hg
Tumia dawa za kupunguza na kushusha presha, kila siku kama ulivyoelezwa na daktari na kama una wasi wasi kuhusu dawa zako ongea na daktari mapema kwa maelezo zaidi.


KWA MSAADA ZAIDI BONYEZA HAPA AU ACHA COMMENT YAKO CHINI
 
















No comments:

Post a Comment

.