Nyama za puani ni nyama laini zilizoota na kuning'inia kwenye njia ya
hewa na mianzi ya pua ambazo husababiswa na uvimbe wa muda mrefu kwenye
mfumo wa upumuaji, pumu, maambukizi ya mara kwa mara, aleji na magonjwa
mengine ya njia ya hewa.
Nyama
zikiwa ndogo huwa hakuna dalili wala ishara zozote zinazoingilia mfumo
wa upumuaji ila zinapokuwa kubwa uzuia hewa kuingia na kuharibu mfumo wa
upumuaji sambamba na kushindwa kunusa, maumivu ya uso, maumivu ya meno
ya juu, mafua, kukoroma, macho kuwasha na maambukizi ya mara kwa mara
katika njia ya hewa.
MATIBABU YAKE
Matibabu
ya tatizo ili huwa ni pamoja na dawa, kubadili mfumo wa maisha na
upasuaji kulingana na ukubwa au visababishi vya tatizo.
Dawa kama nasonex, cetirizine, antibiotiks
huweza kutumika kwa nyia ya kunyunyuzia kwenye pua, vidonge au sindando
ili kupuguza na kuzuia ukuaji wa nyama hizi huku zikisafisha mfumo wa
upumuaji.
Upasuaji
ufanyika endapo dawa zimeshindwa kuondoa tatizo ili na huwa ni upasuaji
wa kutumia hadubini ya ndani kumuongoza daktari kuona kwenye njia ya
hewa na miazi ya pua. Baada ya kufanya upasuaji utaweza kutumia dawa
zilizotajwa juu hapo ili kuzuia kutokea tena kwa tatizo.
Unaweza pia kujitibu kwa kubadili mfumo wa maisha kama nilivyoelekeza katika CHAPISHO ILI
USIPITWE BOFYA HAPA KULIKE PAGE NA WASILIANA NASI FACEBOOK KWA MSAADA NA USHAURI
Naomba kujua kama hizo dawa tajwa hapo juu zinatibu au kutuliza Kwa Muda tu
ReplyDeleteJmn hzo daw hv ni kwel zinaondoa kbx
ReplyDelete