Dakika chache za kwanza unapokutana na mpenzi wako baada ya kuachana kwa kitambo kifupi zinaumuhimu sana.
Kitambo
hiki ni kile ambacho labda mpenzi wako alikuwa kazini au safarini,
umepita muda fulani hamjaonana, yamkini moyoni ulitamani kumuona au
hata kule
kuhisi kumkosa (kummiss) kulishaanza kupoa, jiulize mara utakapomuona,
labda ni uwanja wa ndege, kituo cha basi, au amefungua mlango tu kuingia
nyumbani. Je, unafanya nini? Kile utakachokifanya hapa kina nafasi
kubwa katika kuua taratibu penzi na ukaribu wenu (intimacy) au kulijenga
kwa kasi kubwa. Ni uchaguzi wako, ingawa unashauriwa kufanya haya
yafuatayo:
Jiandae wewe mwenyewe kiakili
Kabla
hamjaonana uso kwa uso andaa vema akili yako kumlaki mpenzi wako.
Fikiri mawazo mazuri na siyo yaliyo mabaya kumhusu yeye. Usiwaze
kummwagia lawama mara tu utakapomwona. Wengine mara tu wamwonapo mpenzi
ameingia huanza kukurupuka kuuliza kama kaja na zawadi, na ole wake
ukute kasahau huo moto utakao waka hapo! Panga nafsini mwako kitu au
tukio la kufurahisha utakalomfanyia mara ukimwona. Mara nyingine unaweza
kumuuliza kwa simu muda atakapowasili ili uweze kujiandaa vile
unavyodhani.
Jiangalie mwonekano wako
Dakika
ya kwanza tu mnapotazamana yaweza kuathiri muendelezo mzima wa siku
yenu. Muonekano wako wa uso, tabasamu lako, harufu yako (nzuri au mbaya)
vyaweza kumdaka au kumkimbiza mpenzi wako, haswa yule wa kiume. wanaume
pia nao wanachakufanya hapa, haupaswi kupokewa ukiwa rafurafu, mchafu,
unatoa harufu mbaya ya mwili au ya viatu. Jiangalie, nywele na ndevu
zako zikoje, meno yako yanaonekanaje na hata ngozi yako hususan ya
usoni. Mwonekano wako huzungumza zaidi vile unavyojiona wewe mwenyewe.
Hauhitaji kusema mimi sijipendi, bali kuonekana kwako kutatoa ujumbe.
Jaribu uwezavyo kuwa mwenye mvuto mara mtakapokuwa na umpendaye.
Onyesha tabasamu la pendo kwa mpenzi wako
Panga
muda wako ili uweze kumsalimu mpenzi wako kwa tabasamu. Acha mpenzi
wako ajue kuwa yeye ni wa kipaumbele, na ni muhimu kwako, usimpokee kwa
staili ya kumwonyesha humjali. Tabasamu linaweza kusema: “I love you”
kuliko hata maneno au zawadi. Tabasamu halina gharama yoyote,
ni la bure na lipo wakati wowote, kinachokushinda kulitumia ni nini?
Hata
kama hujisikii kutabasamu, jitahidi kwa namna yoyote kuonyesha kuwa
unaweza pia kutabasamu. Jifanyishe pale mazingira yanapolazimu, hususan
katika dakika nne za mwanzo. Ikiwa utajifanyisha vizuri, hisia njema
zaweza kuibuka na yale maumivu ya ndani ya moyo kutoweka taratibu.
Salimianeni kwa kukumbatiana na kwa busu
Kuwa
na mtu anayetusubiri mara tutakapofika sehemu au mara tutakapofungua
mlango ni jambo ambalo wengi wetu tunalipenda, kama kubusu siyo mtindo
au pendeleo lako basi tafuta njia nyingine ya miili yenu kugusana mara
mnapoonana. Mfano kushikana mikono, kumshika mwenzako nywele au kichwa,
nk. Mgusano wa mwili ni muhimu na unashauriwa kwa afya ya penzi lenu.
Tengeneza mazingra mwanana
Jipeni
muda wa kupumzika na kupumzisha akili kabla ya kuanza kuzungumzia
matatizo yenu. Kila anayeingia nyumbani nakukuta anapokelewa na makelele
na mikiki mikiki mara nyingi hutamani kuondoka.
Kila
anayekuwa nyumbani kwanza kabla ya mwenzake anawajibika kutengeneza
mazingira ya hisia nzuri, ingawa baada ya hapo wote wawili pia mnawajibu
wa kuendeleza hisia hizi njema na mazingira ya amani yaliyopo.
Wale
ambao wanafanya kazi nje ya nyumbani huhitaji utulivu kidogo mara
wanaporudi ili kutuliza akili na hisia zao, wengine watataka dakika 15
wengine dakika 20, watataka kujinyoosha kidogo, au kusikiliza muziki
fulani bila maongezi mengi, ingawa pia wapo wanaotaka kucheza na watoto
mara wanapofika nyumbani. Chochote na kwa hali yoyote uipendayo, jaribu
kujielezea, na mueleze mwenzako aelewe mtiririko wa hisia zako, hii
itawasaidia sana.
No comments:
Post a Comment