Siku chache baada ya New York na New
Jersey kutangaza utaratibu mpya wa kuwaweka karantini wauguzi na
madaktari waliotoka kuhudumia wagonjwa katika nchi zilizoathiriwa na
Ebola, muuguzi wa kwanza kuathiriwa na utaratibu huo Kaci Hickox
ametishia kufungua mashtaka kutokana na kufanyiwa kitendo hicho.
Muuguzi huyo ameruhusiwa kurejea
nyumbani kwao Maine, ambapo ameilalamikia karantini aliyowekwa mbali na
kutoonekana kuwa na dalili za maambukizi ya Ebola baada ya kuwasili New
Jersey na kutishia kufungua mashtaka kwa kudai kuwa kitendo
alichofanyiwa cha kuwekwa karantini hakikuwa cha kibinadamu na ni
kinyume na haki zake kikatiba.
Marekani inaendelea kuangalia namna
ambavyo itaweza kuweka utaratibu mzuri wa kuwafuatilia kwa ukaribu watu
waliotoka nchi za Afrika Magharibi, Guinea, Liberia na Sierra Leone.
Kituo cha udhibiti wa Magonjwa cha Marekani (CDC) kimetaka kuwepo
utaratibu maalum wa kuwaweka wahudumu wa afya wanaorudi kutoka Afrika
Magharibi katika karantini za nyumbani.
No comments:
Post a Comment