Friday 24 October 2014

KUPONA VIDONDA VYA TUMBO FUATA MAMBO HAYA MUHIMU SANA.

Watu wengi wamekuwa wakilalamika kutopona vidonda vya tumbo baada ya kutumia dawa mbalimbali sababu wamekuwa wakipatiwa dawa ambazo hazitibu kabisa tatizo hilo bali kupunguza maumivu.Baada ya kufanya utafiti kwa muda mrefu sasa suluhisho la tatizo hilo limepatikana na hakuna tena sababu ya kuishi na vidonda vya tumbo. Unaweza kupona Vidonda vya tumbo amabvyo hupatikana kwenye utumbo mdogo (duodenal alcer) na vidonda kwenye tumbo(Gastric ulcers) endepo utafuata mashariti ya fuatayo:



  1. Kuepuka Mawazo kupita kiasi(stress)Kuacha kula vitu vyenye asidi kwa wingi,mf pilipili,limao nk
  2. Kuepuka uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kupita kiasi huchelewesha kupona kwa vidonda
  3. Achana na kula kusikokuwa na mpangilio maalumu na muda maalum.
  4. Unaweza poza maumivu ya vidonda vya tumbo kwa kunywa maziwa na epuka kukaa na njaa muda mrefu
  5. Epuka dawa za Aspirini na NSAIDs 
  6. Epuka unywaji wa kahawa na kashata
  7. Epuka matumizi ya viungo vya vyakula kwa maana hufanya hali kuwa mbaya zaidi.
  8. Unaweza kumuona daktari kama hali inazidi kuwa mbaya ikiambatana na kutapika damu au kukosa choo na maumivu makali juu ya kitovu.
  9. Kwa kuzingatia mambo yafuatayo unaweza kupunguza makali na hatimaye kupona vidonda vya tumbo.
  10. BOFYA HAPA KULIKE PAGE NA WAELIMISHE MARAFIKI 

No comments:

Post a Comment

.