KWA mfano baadhi ya dawa za hospitali huathiri njia ya chakula na
kumsababishia mgonjwa ukosefu wa choo kwa muda mrefu, lakini stafeli
likitumika hurekebisha hali hiyo na kumsaidia mgonjwa kupata choo kama
kawaida.
Vilevile, baadhi ya dawa za hospitali za saratani hudhoofisha
kinga ya mwili, lakini virutubisho vilivyomo kwenye stafeli, hasa
vitamin C, huzifanya kinga kuwa imara na hivyo kuziimarisha hivyo
kumuepusha mtu kupatwa na maambukizi mengine, kama ya njia ya mkojo,
mafua na kikohozi cha mara kwa mara.
FAIDA ZINGINE ZA STAFELI NI KAMA ZIFUATAVYO:
Hutoa nafuu ya kipanda uso.
Kirutubisho aina ya Riboflavin kilichomo kwenye stafeli, husadia kutoa nafuu kwa ugonjwa wa kichwa cha kipanda usoni.
HUZUIA UGONJWA WA ANEMIA
Madini ya chuma (iron) yaliyomo kwenye stafeli, hufaa sana katika kuzuia ugonjwa wa kukauka damu mwilini (anemia).
HUTIBU MAGONJWA YA INI
Juisi ya stafeli inajulikana kwa uwezo wake wa kutibu matatizo ya kwenye ini na uvimbe kwenye kibofu cha mkojo.
HUIMARISHA MIFUPA
Stafeli ni chanzo kizuri pia
cha madini ya kopa (copper) na kashiamu (calcium), virutubisho ambavyo
huwa muhimu kwa ukuaji wa mifupa mwilini.
Matatizo mengine yanayoweza
kudhibitiwa na stafeli ni pamoja na kuumwa miguu, maumivu kwenye
‘joints’, mwili kukosa nguvu na matatizo mengine ya viungo.
MAJANI, MIZIZI, MAGAMBA NAYO NI DAWA
Mbali ya
tunda lenyewe kuwa na faida lukuki kama zilivyoanishwa hapo juu,
vilivyomo vingine kwenye mti huo kama vile mizizi, majani na magamba
yake ni dawa ya magonjwa mbalimbali:
Unywaji wa maji yaliyotengenezwa kutokana na majani ya mstafeli hutibu magonjwa ya ngozi, chunusi na uvimbe wa mwili.
Maji
ya majani ya mstafeli pia hutibu ugonjwa wa kuhara, kukohoa, kuvimba
miguu, mapunye kichwani. Aidha, maji ya majani ya mstafeli yamethibitika
kushusha kiwango cha sukari mwilini.
TAHADHARI
Inaelezwa kwamba stafeli linaweza kuwa
siyo salama kwa wajawazito, wagonjwa wa presha ya kupanda au kushuka
(hypotension or hypertension), hivyo wanashauriwa kabla ya kula, wapate
ushauri wa daktari kwanza.
USHAURI
Kwa asili yake, stafeli lina kiasi kingi
cha virutubisho vinavyoua bakteria, hivyo ulaji wa muda mrefu wa tunda
hili kunaweza kuua bakteria wote tumboni hata wale wazuri, hivyo iwapo
utalila tunda hili kwa zaidi siku 30 mfululizo, unashauriwa pia
kuongezea na dawa za kulainisha njia ya chakula.
JINSI YA KULITUMIA STAFELI
Stafeli linaweza
kuliwa katika aina tofauti. Kama unataka kupata faida zake zote, unaweza
kulila lililoiva kama lilivyo au unaweza kutengeneza juisi yake.
Unywaji wa maji yatokanayo na majani, mizizi au magamba yake, unaweza
kunywa kama chai au kinywaji kingine cha kawaida.
No comments:
Post a Comment