Katika chapisho HILI tuliongelea kuhusu madhara ya vipodozi endapo havitatumika kwa usahihi.
Kabla
hujaanza kutumia vipodozi ni vyema ukajua aina ya ngozi yako kwa
usahihi kabisa na uwezo wa kumudu ghalama za vipodozi kwa muda wote. Hapa lazima ujue kama ngozi yako ni kavu, yenye
mafuta,mchanganyiko ,au una ngozi ambayo ni rahisi kupata chunusi.
Baaada ya kujua aina yako ya ngozi ni vyema ukaingia katika hatua
nyingine ya kuchagua vipodozi vyenye ingredients sahihi kwa ajili ya
ngozi yako. Lakini kwa aina zote za ngozi, vipodozi vyote vyenye
sunscreen na antioxydants ni muhimu sana kwa ajili ya ustawi wa ngozi
yako.
Epuka kutumia vipodozi vyenye ingredients ambazo ni
hatari kiafya na zimepigwa marufuku na serikali, mfano saizi epuka
kutumia vipodozi ambavyo vina kemikali za ‘hydroquinone’ na corticosteroids
Kwa mtu mwenye ngozi
yenye mafuta anatakiwa kutumia vipodozi ambavyo vipo katika’ base’ ya
liquid au gel,ambavyo vinaweza kuwa na ingredients kama vile Benzoyl
peroxide,maji mengi,salicyclic acid na kadhalika, kwa kitaalamu
anatakiwa atumie water based cometics, wakati mtu mwenye ngozi kavu
anatakiwa atumie vipozi ambavyo vina unyevu na mafuta mengi ambavyo
vipo katika ‘base’ ya lotion,cream na kadhalika.
Kwa hiyo
uchaguzi mzuri wa vipodozi ni jambo ambalo kila mtu anapaswa kulijua ili
kupelekea muonekano mzuri, ambao utakuwa mchango mkubwa katika afya ya
mtu kwa namna moja au nyingine.
BOFYA HAPA KULIKE PAGE NA UNGANA NASI FACEBOOK KWA MSAADA ZAIDI
No comments:
Post a Comment