Saturday 11 October 2014

LISHE NA FAIDA KUMI UNAZOPATA KUTOKANA NA KULA MAYAI.

Mayai yana kiwango kikubwa cha virutubisho na madini ambayo ni muhimu sana kwa afya yako.  Hivi ni baadhi ya virutubisho vinavyoweza kuujenga mwili wako asa unapokula yai walau wara chache kwa wiki;-

 1. Mafuta ya omega-3 husaidia afya ya ubongo na macho.

2. Protini husaidia kujenga misuli, viungo, ngozi, tishu na homoni mwilini.
3. Vitamini A husaidia afya ya ngozi, kinga ya mwili na kuona vizuri.
4. Vitamin B2, B5 na B12 husaidia matumizi ya nguvu na chakula kilichopo mwilini, mfumo wa damu na fahamu kufanya kazi vizuri.
5. Vitamini D huboresha afya ya mifupa na meno pamoja na kufyonzwa kwa madini ya kalsiumu tumboni.
6. Vitamini E, huimarisha afya ya misuli, mfumo wa fahamu na uzazi.
 7. Cholini, husaidia matumizi ya mafuta mwilini na kuboresha afya ya ini.
8. Folic asidi husaidia kukua kwa misuli, tishu na kutengenezwa kwa damu asa kwa wajawazito.
Lutein, husaidia kuona vizuri na kuzuia kuzeeka haraka.
10.  Virutubisho vingine ni pamoja na selenium, phosphorus, iodine, chuma, biotin n.k ambavyo kwa pamoja hushirikiana kuimarisha afya yako.
BOFYA HAPA NA LIKE PAGE KUJUA MENGI ZAIDI. 

No comments:

Post a Comment

.