Hata hivyo, watafiti nchini Marekani wamebaini kuwa wanawake
wanaokunywa juisi ya nyanya angalau mara moja kwa wiki, wanapunguza
kiwango cha kupata maradhi ya saratani ya matiti.
Kwa mfano, wanaeleza kuwa glasi moja ya nyanya kwa siku ina kiwango
sahihi na cha kutosha cha madini ya Lycopene, ambazo ni kemikali za
mimea zinazoamnika kuondoa kukua kwa saratani.
Madini ya Lycopene ndiyo yanayozipa nyanya rangi yake nyekundu na
nyanya hizo zimeundwa zaidi ya vichocheo vyenye uwezo wa kuzuia saratani
hiyo.
Watafiti katika Chuo Kikuu cha Rutgers nchini Marekani walipima,
kiwangon cha vichocheo kwa wanawake 70 wenye miaka 55 na kuendelea ambao
walitumia juisi ya nyanya kwa wiki kumi. Wanawake hao ambao wengi
walikuwa wanene kupita kiasi na baadhi wenye dalili ya saratani,
walipungua uzito na saratani ilikwisha.
Kwa kuwa nyanya ni tunda linalopatikana wakati wowote, tena jikoni
kwako, ni vyema wanawake wakajenga mazoea ya kuzitumia kama mlo hata
wasipotengeneza juisi.
source: Mwananchi
BOFYA HAPA NA LIKE PAGE KUJUA MENGI ZAIDI.
source: Mwananchi
BOFYA HAPA NA LIKE PAGE KUJUA MENGI ZAIDI.
No comments:
Post a Comment