Tuesday 7 October 2014

FAHAMU MAPEMA KUHUSU MAAMBUKIZI NA UVIMBE KATIKA TANDO ZA UBONGO(Meningitis)

Uvimbe katika utando wa ubongo au uti wa mgongo ni miongoni mwa magonjwa hatari sana ambao huua haraka. Ugonjwa huu hushambulia ubongo na uti wa mgongo hasa kwa watoto wadogo na husabababishwa na maambukizi ya bakteria, virusi na fangasi.
Unaweza kuanza kama tatizo la ugonjwa mwingine kama vile surua, kifaduro, kukohoa au malaria hivyo ni muhimu sana kumuwaisha mgonjwa hospitali kwa ajili ya matatibabu ili kuepuka madhara zaidi kama ulemavu wa kudumu, kifo, kifafa mshtuko na magonjwa ya akili. 

Dalili na ishara.
Ugonjwa huu hutambulika kwa dalili zifuatazo. 
Homa na kuchanganyikiwa kwa akili.
Kutoweza kustahimili mwanga na kelele.
Maumivu makali ya kichwa.
Mkazo wa shingo.
Mgongo kupinda kwa nyuma. 
Kwa watoto walio na umri chini ya mwaka mmoja utosi uvimba wakati mwingine degedege hutokea au kujitupatupa ovyo ovyo na hali inavyoendelea kuwa mbaya hupotewa na fahamu.
Tiba na jinsi ya kujikinga au kumkinga mwanao.
Ugonjwa huu hutibiwa kutokana na visababishi ambapo dawa kwa ajili ya kuua maambukizi, degedege, kupunguza uvimbe kwenye ubongo, dripu za maji na chakula, dawa za kutuliza homa na maumivu hutolewa kwa maelekezo ya daktari mpaka mgonjwa atakapopata nafuu.
Pia tahadhari inabidi zichukuliwe kwa kuepuka maambukizi kwa njia ya hewa, kufanya usafi, kutoshirikiana vifaa vyenye ncha kali au mswaki na mgonjwa, kufunika mdomo wakati wa kukohoa, lishe bora inayoongeza kinga ya mwili na kupata chanjo ya ugonjwa huu hasa za MCV4 na MPSV4 kwa watoto wadogo.
LIKE PAGE NA WASILIANA NASI FACEBOOK KWA MSAADA ZAIDI NA USHAURI. 
 
 .

No comments:

Post a Comment

.