Thursday 23 October 2014

MAMBO YA KUFANYA ILI USIPATE CHUNUSI

Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujit-okeza kama viuvimbe/vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso,kifuani na hata mgongoni.Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani Bacteria. Unaweza kufanya yafuatayo ili kuepuka swala la chunusi usoni ambalo uharibu urembo wa ngozi yako.
1.    Osha taratibu sehemu unayodhani ina chunusi kwa maji safi na sabuni angalau mara mbili kila siku huku ukisugua taratibu ,usikwaruze kwa kucha au kitu choichote kigumu.

2.  Tumia make-up au vilainisha ngozi visivyo na mafuta mgando
 
3.  Osha nywele zako kila mara na epuka nywele kuziba uso (kwa wenye nywele ndefu)

4.  Kula mlo kamili na epuka vyakula vyenye mafuta mengi.

5.  Usibinye au kutoboa vipele kwa pini au kitu chenye ncha kali.

6.  Epuka kukaa sana juani,mwanga wa asubuhi ni mzuri ili kupata vitamin D

7.  Punguza mawazo 
8. Pia unaweza kupaka mask za asali, mayai, sabuni na asali kwa muda wa masaa 4 ili kusaidia ngozi yako kuwa laini.

No comments:

Post a Comment

.